• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utawala kwa mujibu wa sheria waleta sura mpya katika utawala wa nchi ya China

    (GMT+08:00) 2015-02-28 19:25:49

    Gazeti la Renminribao la China limechapisha makala ya mhariri inayoelezea umuhimu wa kutawala nchi kwa mujibu wa sheria.

    Makala hiyo inasema tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike mwishoni mwa mwaka 2012, kutawala nchi kwa mujibu wa sheria na kufanya mageuzi ya kina zimekuwa zikifanya kazi kama magurudumu yanayosukuma maendeleo ya China.

    Utawala kwa kufuata sheria ni mabadiliko makubwa yanayoibuka katika historia ya China ambayo utawala wake ulikuwa unategemea mtu mmoja mmoja kwa muda wa karne kadhaa.

    Hatua hiyo ya kimkakati ya kutawala nchi kwa sheria ikiwa ni pamoja na kufanya mageuzi ya kina na kuendesha chama kwa kufuata nidhamu kwa makini zimeweka msingi na hakikisho kwa lengo la kujenga jamii yenye maisha bora. Utawala kwa kufuata sheria pia umeweka msingi imara kwa mageuzi yoyote makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako