• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upigaji kura wa uchaguzi mkuu waanza nchini Lesotho

    (GMT+08:00) 2015-02-28 19:42:20

    Raia wa Lesotho leo wamejitokeza mapema kwenye vituo vya kupigia kura kushiriki kwenye uchaguzi mkuu unaolenga kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

    Uchaguzi huo umefanyika miaka miwili mapema kuliko livyopangwa kutokana na makubaliano ya kisiasa kati ya vyama mbalimbali vya kisiasa nchini humo kwa upatanishi wa jumuiya ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC.

    Lesotho ilitumbukia katika msukosuko wa kisiasa tangu Juni mwaka jana baada ya waziri mkuu Thomas Thabane kuvunja bunge ili kuepuka kura ya kutokua na imani naye iliyokuwa ikishinikizwa na washirika wake wa serikali ya muungano. Agosti mwaka jana, mapinduzi ya kisiasa dhidi ya Thabane yalizuiliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako