• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba watarajiwa kurudishwa Aprili

    (GMT+08:00) 2015-02-28 19:46:15

    Mazungumzo ya duru ya pili kati ya Marekani na Cuba yanayolenga kurudisha uhusiano wa kidiplomasia kati yao yamepata maendeleo makubwa. Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Roberta Jacobson amesema nchi hizo mbili zinatarajiwa kufungua tena ofisi za ubalozi mwanzoni mwa mwezi April kabla ya mkutano wa viongozi wa jumuiya ya nchi za Amerika.

    Katika hatua ya kuboresha uhusiano wake na Cuba, Marekani iliondoa baadhi ya vikwazo dhidi ya Cuba Desemba mwaka jana. Maofisa wa kidiplomasia wa nchi hizo mbili walifanya mazungumzo ya kwanza mjini Havana na kubadilishana maoni kuhusu masuala ya uhamiaji, kurudisha uhusiano wa kidiplomasia na kufungua tena ofisi za ubalozi.

    Katika duru hiyo ya mazungumzo, Cuba imeitaka Marekani iondoe jina lake kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi. Marekani imesema inatathmini ombi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako