• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutilia maanani zaidi utekelezaji wa sheria kuhusu uhifadhi wa mazingira

    (GMT+08:00) 2015-03-03 17:58:46


    Naibu waziri wa mazingira wa China Pan Yue amesema, mwaka huu, China itatilia maanani utekelezaji wa sheria kuhusu uhifadhi wa mazingira na kuzindua njia ya kukusanya habari kupitia simu za mikononi.

    Pan amesema, mwaka huu wizara ya uhifadhi wa mazingira itaongeza juhudi kushughulikia ujenzi wa miradi bila ya kibali na kutoa adhabu kwa wahusika wa miradi ambayo inaleta athari kwa mazingira.
    Amesema katika miezi miwili iliyopita tangu sheria mpya ya uhifadhi wa mazingira ianze kutekelezwa, faini zaidi ya dola za kimarekani milioni 1 zimetozwa, huku miradi zaidi ya 200 imesitishwa. Ameongeza kuwa mahakama maalum zaidi ya 300 zinazoshughulikia kesi za uhifadhi wa mazingira zimeanzishwa katika mikoa 18 nchini China.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako