• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Bw Riek Machar wakutana Addis Ababa

    (GMT+08:00) 2015-03-04 09:54:26

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na aliyekuwa makamu wake Bw Riek Machar, jana mjini Addis Ababa walikutana ikiwa ni sehemu ya juhudi za upatanishi zinazofanywa na jumuiya ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD, wakati muda wa kukamilisha mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini unapokaribia kufika mwisho.

    Kutokana na juhudi za IGAD mkutano wa mwisho kuhusu mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini ulianza Februari 23, ikiwa ni sehemu ya upatanishi wa jumuiya hiyo kumaliza mgogoro wa Sudan Kusini ulioanza mwezi Desemba mwaka 2013. Rais Kiir na Bw Machar tarehe Mosi Februari walikubaliana kukamilisha mazungumzo tarehe 5 Machi, na kuanza kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa kabla ya tarehe 9 Julai. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, kipindi kabla ya kuanzisha serikali ya mpito kinatakiwa kuanza April 1.

    Wakati huo huo China inaendelea kuzihimiza pande zinazopambana kuacha mapigano, na kuunda serikali ya mpito haraka iwezekanavyo. Mjumbe wa kudumu wa China kwenye umoja wa mataifa Bw Liu Jieyi amesema kwenye mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuwa China inatumai kuwa pande mbili zitafikia makubaliano haraka kuhusu mambo yaliyobaki, ili zichukue hatua kurudisha amani na utulivu kwa kuwa hayo ni maslahi ya kimsingi na ya muda mrefu kwa Sudan Kusini na wananchi wake.

    Wakati jumuiya ya kimataifa ikiendelea na juhudi za upatanishi, baraza la usalama la Umoja wa mataifa jana lilipitisha azimio kuwawekea vikwazo wale wanaotishia amani, usalama na utulivu wa Sudan Kusini. Baraza hilo lilipitisha azimio hilo kwa kauli moja kuweka vikwazo vya kusafiri na kuzuia mali za watu au makundi yanayohusika na vitendo na sera zinazoweza kuzuia amani ya Sudan Kusini.

    Vikwazo pia vitawalenga wale wenye lengo la kueneza mgogoro wa Sudan Kusini, kukwamisha mchakato wa amani na mazungumzo, na wanaokiuka makubaliano ya kusimamisha uhasama yaliyosainiwa kati ya serikali na upinzani. Baraza la usalama pia limeunda kamati ya wajumbe watakaosimamia utekelezaji wa vikwazo, na kuripoti kazi yake kwa baraza hilo ndani ya siku 60.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako