• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shinikizo la kiuchumi kwa vijana wa China wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China

    (GMT+08:00) 2015-03-04 15:13:32
    A Wasikilizaji wapendwa, karibuni katika kipindi cha uchumi na maendeleo. Mimi ni Carol.

    B Mimi ni Fadhili.

    A Likizo ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China imemalizika, watu wote wamerudi kazini. Kwenye ofisi yetu kuna vyakula vingi vilivoletwa na wenzetu kutoka nyumbani mwao. Nina imani kuwa wana furaha kubwa katika likizo hiyo.

    B Ndiyo. Lakini licha ya furaha, nafikiri pia wanachoka.

    A Wanachoka? Hakika walikuwa wanacheza sana.

    B Ndiyo. Nimewauliza wenzetu wa China jinsi walivyopita likizo ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Ni kama tulivyojulisha katika vipindi maalumu vilivyotangazawa siku kadhaa zilizopita, baadhi yao walikwenda tamsha la Miaohui hapa Beijing, wengi wamerudi nyumbani kwao na kupita likizo pamoja na wazazi wao. Na mwenzetu mmoja ametalii barani Ulaya.

    A Ndiyo. Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China ni muhimu sana kwa wachina, katika kipindi hicho wachina husalimiana na kutembeana. Jamaa na marafiki waliokuwa wanashindwa kukutana mara kwa mara katika mwaka mzima uliopita, wanakutana kula chakula na kunywa pombe pamoja. Ingawa wanachoka, lakini wanafurahi, sivyo?

    B Haha, watu kadhaa wana malalamiko kuwa ingawa wanafurahi sana, lakini pia wanachoka sana. Baadhi ya vijana wamesema, kurudi makwao na kupita sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China ni mzigo mzito, hasa kwa upande wa uchumi.

    A Nakubali. Miezi miwili kabla ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, wenzetu wa China wameanza kuagiza tiketi za treni au ndege, kama wasingeagiza tiketi za treni kwa wakati, wangeshindwa kununua tiketi za kurudi nyumbani. Na kama wakiagiza tiketi za ndege mapema, wanaweza kununua tiketi hizo kwa bei nafuu. China ni nchi yenye ardhi kubwa sana, nafikiri pesa zilizotumika katika kwenda na kuja hakika zimechukua sehemu kubwa katika gharama za kupita likizo ya sikukuu ya mwaka mpya wa jaddi wa China.

    B Bila shaka tikiti za kwenda makwao na kurudi hapa zinahitaji pasa, ambazo si thamani ndogo. Lakini je, huelewi desturi ya wachina kuhusu kupita sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China? Licha ya pesa zilizotumika katika gharama ya mawasiliano ya barabara, pesa zilitotumika katika mawasiliano ya watu ndiyo gharama kubwa zaidi.

    A Pesa zitatumika katika mawasiliano ya watu? Vipi?

    B Tuseme wewe umeondoka nyumbani kwa muda mrefu, na hujakutana na wazazi wako kwa muda mrefu, sasa unarudi nyumbani na kupita likizo ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China pamoja nao, utanunua zawadi kwa wazazi wako au la? Zawadi mfano wa nguo mpya. Aidha, usisahau dada na kaka zako na watoto wao, lazima uzingatie kila mtu. Zawadi kwa watu hao ni gharama kubwa. Licha ya hayo, baada ya kurudi nyumbani, hakika utakutana na marafiki wa zamani, na nyinyi mtakula chakula na kunywa pombe mkahawani. Wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, wachina wana mila ya hutoa pesa kwa watoto, kwa kichina pesa hizo zinaitwa Hongbao, pesa hizo ni kubwa kwa jumla.

    A Ndiyo. Niliwahi kusoma habari hivi karibuni, kwamba watu wengi wameamua kutorudi nyumbani katika likizo ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, kutokana na shinikizo la kiuchumi.

    B Ndiyo. Takwimu husika zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni iliyopita, gharama za kupita sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China zinaongezeka. Tiketi za treni ambazo ni vigumu kununuliwa, safari ndefu za kurudi nyumbani na pesa nyingi zinazotumika katka mawasiliano ya watu, zote zimekuwa mizigo mizito kwa watu wanaofanya kazi katika miji mikubwa.

    A Habari niliyosoma inasema, mama Wang anayefanya kazi za vibarua mjini alikuwa harudi maskani yake ya vijijini wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China kwa miaka kadhaa. Amesema anaogopa kama akirudi na kupita sikukuu hiyo, atalazimika kutumia pesa karibu na mapato yake ya mwaka mmoja, atalazimika kununua zawadi kwa jamaa zote, pia atalazimika kutoa pesa kwa watoto wa jamaa. Na jamaa zake wanaona kuwa mama Wang anafanya kazi kaitka mji mkubwa, si vizuri kutoa pesa chache.

    B Baadhi ya wachina wamependekeza kuwa raia wa kawaida wanapaswa kupata mamlaka ya kuamua likizo, ili kupata fursa nyingi zaidi ya kurudi nyumbani. Hasa katika kipindi cha sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, wachina wanaweza kuamua safari zao kwa mujibu wa mahitaji yao. Hivyo watu wengi hawana haja ya kutumia pesa nyingi katika kipindi hicho tu.

    A Sawa, sasa tupate burudani kidogo ya muziki kabla ya tusikilize jinsi baadhi ya wenzi wetu wa China walivyopita sikukuu hiyo, na walitumia pesa ngapi.

    A:Je, watu wanatumia pesa ngapi katika likizo ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China? Nadhani kutokana na maeneo, mapato na njia tofauti ya kupita sikukuu, matumizi ya fedha hakika ni tofauti. Baadhi ya wenzi wetu wamepita likizo hii kwa njia tofauti. Grace alikaa hapa Beijing tu, Laowu na mkewe na mtoto wake walikwenda maskani yake kukutana na jamaa zake mkoani Jiangsu, Upendo na mumewe walikwenda kufanya utalii nchini Ufaransa, Italia na Uswisi.

    Sasa

    B: Sasa tusikilize jinsi walivyopita likizo yao, ili kujua walitumia fedha ngapi.

    Grace: Mimi ni Grace, maskani yangu ni mkoa wa Jiangsu, umbali wa kilomita 1,200 hivi kutoka hapa Beijing. Likizoni nilikaa Beijing tu kwa sababu mimi ni mjamzito, si busara kusafiri ndefu kwa treni. Kwa hiyo matumizi ya fedha ni madogo kuliko yale ya zamani nilipokwenda Jiangsu. Wazazi wakwe walikuja Beijing, pesa nyingi zilitumiwa kununua vyakula, tulinunua vyakula vingi na vizuri zaidi ili kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China. Jamaa zangu pamoja na watoto watatu wao pia walikuja Beijing kututembelea, baadhi ya siku tulikula pamoja mikahawani, pia tuliwapa watoto wao yuan 500 kila mmoja kama ni zawadi. Katika likizo hii kwa ujumla tulitumia yuan 5000 hivi, sawa na dola za kimarekani 830.

    Lao Wu: Mimi ni Lao Wu, likizo hii nilirudi maskani yangu mkoani Jiangsu pamoja na mke wangu na binti yangu. Nilitoa yuan 4500 katika kununua tiketi za treni, kwani tulishindwa kununua tiketi za viti vya kawaida, ili kurudi nyumbani kwa wakati, tulinunua tiketi za viti vya ngazi ya juu, hivyo pesa zilizotumika katika tiketi za treni zimeongezeka kwa mara moja kuliko hali ya kawaida. Na nina dada wanne, kila dada ana mtoto mmoja, na nilitoa yuan 1000 kwa kila mtoto. Licha ya hayo nilinunua zawadi kwa wazazi wangu na jamaa wengine. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa binti yangu kupita sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China katika mkoa wa Jiangsu, hivyo nilimwongoza kutembelea sehemu mbalimbali, mtoto alitaka zawadi na toy nyingi, hivyo niligharimu sana katika vitu hivyo. Kwa jumla nilitoa yuan zaidi ya 15,000 katika likizo hiyo, sawa na dola za kimarekani 2,490.

    Upendo: Mimi naitwa Upendo. Katika likizo ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China mimi na mume wangu tulikwenda Ufaransa, Italia na Uswiss kwa wiki mbili. Gharama ya safari hii ni kubwa, tiketi ya ndege Euro 2000, hoteli Euro 2000, Chakula tulitumia karibu Euro 800, mchana tulikula hamburger na Sandwich, na jioni tulikwenda mkahawa mkubwa, kwa kuwa chakula ni ghali, katika mkahawa mkubwa gharama kwa kila mtu ni karibu Euro 30, hatukwenda mkahawa mkubwa mara kwa mara. Vilevile tulinunua zawadi kwa ajili ya jamaa na marafiki yetu. chocolate zinazotengenezwa nchini Uswiss ni maarufu, kwa hiyo tulinunua nyingi gharama yake ni karibu Eruo 400.

    A: Lo!

    B: Umeshangazwa?

    A: Ndiyo, lakini sasa najua kwanini baadhi ya vijana hawataki kwenda maskani yao katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, kwa sababu matumizi ya fedha ni makubwa.

    B: Kabla ya sikukuu ya mwaka mpya tovuti moja ilifanya uchunguzi kwa kuwauliza watu wasiofanya kazi katika maskani yao. Baadhi ya watu walioulizwa walisema hawaendi maskani yao likizoni. Sasabu kubwa zaidi ni kwamba hawajapata mafanikio makubwa katika kazi, hivyo wanaona aibu wakirudi maskani yao. Sababu ya pili ni gharama kubwa zinazopaswa kutumika wakati wa sikukuu hii. Sababu ya tatu ni tatizo la kusafiri. Wachina wana sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, na Waafrika wana sikukuu ya Krismas. Caro, unaweza kuniambia unapita vipi sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China? Umetumia fedha ngapi? Sikukuu hiyo ina tofauti gani na sikukuu ya Krismas nchini Tanzania?

    A Nimekuwepo nchini China kwa takriban miaka mitano sasa, na nimesherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China kwa miaka minne. Binafsi, kwa kuwa ni mgeni katika nchi hii, sikuwa na matumizi makubwa sana. Nilitoka na marafiki zangu kwenda kula mgahawani na kuangalia fataki, na pale nilipoweza, niliwanunulia marafiki zangu zawadi kama vile chocolate kwa ajili ya sherehe hii.

    Tofauti na nyumbani Tanzania, kule kuna sikukuu ya Krismas na mwaka mpya. Kusema kweli sikukuu hizo huwa zinaongeza matumizi, na kama mtu hana akiba, mambo yanaweza yasiwe mazuri kwa upande wako. Wakati wa sikukuu ya Krismas, kwa upande wangu nilitakiwa kuhakikisha mtoto wangu anapata nguo mpya, anaenda kutembea kwenye sehemu nzuri zinazovutia, na pia anapata kuwaalika marafiki zake kwa ajili ya chakula na vinywaji baridi. Pamoja na kuhakikisha kuwa mtoto wangu anafurahia sikukuu, bado kuna majukumu ninayotakiwa kutimiza kama sehemu ya familia. Tunakutana na kula pamoja kama familia, hivyo hapo pia kila mtu anakuwa na sehemu yake anayotakiwa kuitimiza. Licha ya hayo, kuna watoto wa dada na kaka ambao furaha yao ni kupata japo zawadi ndogo kutoka kwa shangazi yao. Kwa maana hiyo, kama mtu hujajipanga mapema, sikukuu inaweza kuwa mbaya.

    B Kuhusu tatizo la matumizi ya fedha katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, nadhani watu wanatakiwa kutumia fedha kwa mujibu wa uwezo wao, kutunga mpango kabla sikukuu hiyo, na kununua vitu vya kusherehekea sikukuu hiyo na kutoa zawadi kwa mujibu wa hali zao tofauti. Jamaa wanapenda zaidi kusherehekea pamoja sikukuu badala ya kupata zawadi.

    A: Nakubali. Kusherehekea pamoja ni muhimu zaidi kuliko zawadi. Hivyo nadhani watu wanatakiwa kununua zawadi kwa mujibu wa uwezo wao. Likizoni ni bora tupumzike vizuri, kukutana na wazazi, jamaa na marafiki zetu badala ya kutumia fedha ovyo.

    B: Baadhi ya watu wanasema hawana hamu kubwa ya kupita sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Sababu kubwa ni kwamba wana matarajio makubwa zaidi kuhusu sikukuu hiyo, wanatumia fedha nyingi zaidi bila kujadi mapato yao. Baada ya kununua vitu vingi, wanaona shinikizo kubwa, na furaha yao inapungua. Baadhi ya wataalamu waliwashauri watu watilie maanani zaidi utamaduni wa mwaka mpya badala ya kununua zawadi tu.

    A: Ndiyo, watu watafikiria zaidi watakapotumia fedha, wataacha njia ya zamani kutumia fedha nyingi kupita kiasi. Sasa Wachina wana uwezo mkubwa zaidi, na wanatumia fedha nyingi zaidi siku hadi siku, lakini wanatakiwa kutilia maanani utamaduni wa jadi wa China badala ya kutumia pesa ovyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako