• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajenda za mkutano wa tatu wa bunge la awamu ya 12 la umma la China zathibitishwa

    (GMT+08:00) 2015-03-04 15:30:33

    Mkutano wa maandalizi ya mkutano wa tatu wa bunge la awamu ya 12 la umma la China umefanyika leo asubuhi hapa Beijing na kuendeshwa na spika wa bunge hilo Zhang Dejiang.

    Mkutano huo umethibitisha ajenga za mkutano wa bunge la umma utakaoanza kesho.

    Ajenda hizo ni pamoja na kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali, kukagua na kuidhinisha utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii kwa mwaka 2014 na mswada wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii kwa mwaka 2015, kukagua utekelezaji wa bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa ya mwaka uliopita na kupitisha bajeti za mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako