Upendo usiokuwa na mipaka Tangu China ilipotuma kikundi cha madaktari barani Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1963, China imeendelea na kazi hiyo kwa miaka 51. Mwaka 2013 Rais Xi Jinping alipokutana na ujumbe wa madaktari hodari waliotoa msaada wa matibabu nchi za nje alisema, kutoa msaada wa matibabu ni sehemu muhimu ya diplomasia ya China, madaktari wa China si kama tu wamehimiza maendeleo ya jukumu la afya la nchi walipotoa msaada na kuinua kiwango cha afya za watu wa huko, bali pia wamehimiza urafiki kati ya wananchi wa China na nchi nyingine.
|