• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa ujenzi wa reli inayojengwa na kampuni ya China wachangia maendeleo ya jamii ya Wakenya

    (GMT+08:00) 2015-03-12 10:27:00

    Mradi wa ujenzi wa reli yenye urefu wa kilomita 472 unaofanywa na kampuni ya China umepata mafanikio makubwa tangu uanze Januari mwaka huu, huku kampuni inayosimamia mradi huo CRBC ikitekeleza miradi mbalimbali ya kijamii.

    Takwimu zinaonyesha kuwa, idadi kubwa ya Wakenya wamepata ajira baada ya mradi huo kuanza kutekelezwa, ambapo kwenye kaunti ya Makueni zaidi ya wakazi 3000 wameajiriwa katika kampuni hiyo. Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Matangini iliopo Mangelete ameishukuru kampuni hiyo kwa kukarabati majengo ya shuleni. Kampuni hiyo pia imechangia saruji, mbao, na fedha ili kusaidia ujenzi wa mabweni katika shule ya upili ya Molemuni iliyopo kwenye kaunti ya Makueni.

    Wakati huohuo, kampuni hiyo imewasaidia wakazi wa kijiji cha Ulu kukarabati barabara yenye urefu wa kilomita 8.3 ambayo ilikuwa imeharibika kwa kutoa fedha, wataalam, na vifaa kwa ajili ya ukarabati huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako