• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujisomea kuna manufaa makubwa kwa jamii yote

    (GMT+08:00) 2015-03-19 14:38:47

    Toka mwaka huu uanze nimekuwa nasoma kitabu kimoja kinachohusu utamaduni wa jadi wa China, nasoma kitabu hiki ili kuongeza uelewa wangu kuhusu China na wa China. Bahati nzuri ni kuwa wakati nasoma kitabu hiki, umetolewa mwito kuhusu usomaji vitabu hapa China. Wakati hilo linazungumzwa, nilijaribu kuangalia hali ya usomaji wa vitabu kwenye nchi zetu za Afrika, na kupata maoni kutoka kwa Bw Peter, mkutubi kutoka Tanzania aliyeeleza hali ya usomaji wa vitabu nchini Tanzania


    Pili: Kabla ya kuzungumzia hali ya hapa China kuhusu usomaji wa vitabu, ni vizuri tukiwafahamisha wasikilizaji kuwa kwenye ripoti ya kazi za serikali ya mwaka jana iliyowasilishwa na waziri mkuu kwenye mkutano wa bunge la umma la China uliofungwa wiki iliyopita, kwa mara ya kwanza suala la kuwahimiza wananchi wajisomee vitabu limewekwa kwenye ripoti. Wametumia maneno kujenga "Jamii yenye harufu nzuri ya vitabu", kwa tafsiri ya haraka ni kwamba vitabu vizuri vinapatikana kwa wingi, watu wanapenda kusoma vitabu, na kuna mazingira mazuri ya usomaji wa vitabu. Kwa ujumla ni kuwa wananchi wawe moyo wa kupenda kusoma vitabu, na wawe wanasoma vitabu vyenye manufaa.

    Fadhili: Nakumbuka huko nyuma tumewahi kuzungumzia suala la usomaji wa vitabu. Hapa China tunafahamu kuwa kuna utamaduni mkubwa wa kujisomea, ingawa siku hizi labda si sahihi sana kutumia tafsiri ya jadi ya usomaji, na kusema usomaji wa vitabu. Siku hizi watu wanaweza kusoma kwenye mtandao wa Internet, kwenye simu zao na hata kwenye vifaa vingine vya kisasa vya kusomea kama Ipad, kindle na vingine. Lakini kimsingi ni kuwa lile wazo la kujisomea liko palepale.


    Pili: Tulioko hapa Beijing tunaona kuwa wachina ni wasomaji wazuri, lakini tukiangalia kwa ujumla ikilinganishwa na watu wa nchi nyingine duniani wachina bado wako nyuma. Tukiangalia takwimu zilizotolewa shirika la elimu na sayansi na teknolojia la Umoja wa mataifa UNESCO, zinaonesha kuwa waisrael wanasoma vitabu 64 kwa mwaka, wajapan wanasoma vitabu 40 kwa mwaka, wamarekani wanasoma vitabu 21, wafaransa wanasoma 20. Lakini mwaka jana wachina walisoma wastani wa vitabu vinne tu kwa mwaka, idadi hii ni asilimia 10 ya idadi ya vitabu vinavyosomwa na watu wa nchi zilizoendelea


    Fadhili: Takwimu hizo kwa upande wa China si za kuridhisha, na sisi tunaoishi hapa China tunaona kuwa mijini watu ndio wana mazingira ya kusoma, lakini watu wa vijijini hawana mazingira mazuri kama watu wa mjini, lakini hata watu wa mjini pia wana changamoto za pilika nyingi za maisha hasa kazi, kwa hiyo hali halisi ni kuwa hata kama una moto wa kujisomea mazingira hayaruhusu sana usome vitabu vingi kama watu wa Israel.


    Pili: Hali hiyo ya pilika za maisha inaathiri kwa kiasi fulani usomaji wa vitabu. Lakini umuhimu wa kusoma vitabu uko pale pale, ndio maana kwenye mkutano na waandishi wa habari waziri Mkuu Bw Li Keqiang alikumbusha kuwa kujisomea ni moja ya njia ya kurithisha utamaduni wa binadamu. Pia amesema kujenga tabia ya kujisomea vitabu, na kuiunganisha na njia ya kufanya kazi, siyo tu itasaidia kuongezeka kwa uwezo za ubunifu, bali pia itaongeza nguvu za maadili katika jamii. Na hii ndio sababu ya serikali ya China kutaja suala la kuwahimiza wananchi wajisomee kwenye ripoti ya kazi za serikali kwa mwaka jana na mwaka huu.


    Fadhili: Katika hali ya kawaida tunaweza kusema kuwa viongozi wakubwa wanapaswa kuzungumzia mambo makubwa yanayohusu uchumi wa nchi au ajira, usalama, na haya mengine labda yanaweza kuzungumzwa na viongozi wengine wa ngazi ya chini. Lakini jambo hili kuzungumzwa na waziri mkuu inaonesha kuwa serikali ya China iko makini katika kuhakikisha utamaduni wa kujisomea unarithishwa, na pia inaonesha kuwa haifurahishwi na takwimu za UNESCO zinazoonesha kuwa China bado iko nyuma sana ikilinganishwa na nchi zilizoendelea. Na sio viongozi wakubwa tu, hata wawakilishi wa bunge la umma pia nao wamezungumzia jambo hilo, kama anavyoeleza mwakilishi Bibi Huang Xihua
    Sauti
    "Kujisomea vitabu kunaleta manufaa makubwa kwa jamii yote kiasi kwamba hayawezi kupimwa kwa fedha, kunasaidia kutengeneza tabia nzuri ya jamii nzima na vizazi vijavyo. Kujisomea vitabu kunapaswa kuhimizwa, kama ukisoma, bila kujali unasoma kitabu cha aina gani, kutakuwa na manufaa."


    Pili: Mwakilishi huyu anaeleza vizuri kuwa kusoma ni muhimu, lakini hali halisi ya maisha ya sasa hapa China imeleta ugumu. Pamoja na kuwa takwimu za UNESCO zinaonesha kuwa watu wa nchi nyingine wanasoma vitabu vingi zaidi, nimebahatika kutembelea baadhi ya nchi hizo kwa kweli mazingira yake ni tofauti sana na mazingira ya China hasa sehemu za mjini. Naweza kutoa mfano mmoja, kwenye nchi za Ulaya watu wakiwa kwenye subway wanaweza kusoma vitabu, lakini hapa Beijing hasa asubuhi na jioni ukiwa kwenye basi au subway msongamano ni mkubwa na huwezi kusoma, au kwa ufupi pilika na maisha kwenye miji ya China ni nyingi na hazitoi muda wa kutosha kusoma vitabu vingi.


    Fadhili: Kutokuwepo kwa muda wa kutosha kujisomea kumefanya baadhi ya miji hapa China kuchukua hatua ya kuhimiza watu kujisomea. Mfano mzuri ni mji wa Shenzhen, uliopo kusini mwa China, mji huu ni moja ambao kwa muda wa miaka 15 sasa unahimiza watu kujisomea. Kuanzia mwaka 2000, serikali ilitangaza mwezi Novemba kuwa mwezi wa kujisomea. Katika miaka 15 iliyopita, idadi ya wanaoshiriki kwenye shughuli ya mwezi wa kujisomea iliendelea kuongezeka kutoka milioni 1.7 ya mwaka wa kwanza hadi zaidi ya milioni 10. Mwaka 2013 UNESCO ilitoa tuzo kwa mji huo kuwa "Mji wa kuigwa ya kuhimiza watu wasome"


    Pili: Mbali na kuwa na mwezi wa kujisomea pia kuna shughuli nyingine za kuhimiza usomaji wa vitabu, kama anavyoeleza Bibi Song Lijuan ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa klabu moja ya kujisomea vitabu
    Sauti
    "Kuna shughuli moja iitwayo kupokezana vitabu. Yaani ukimaliza kusoma kitabu, unampa rafiki yako, rafiki yako akimaliza naye anampatia rafiki yake. Kuna kitabu kimoja kilichozunguka hadi Marekani na Canada."
    Pili: Hii ni moja ya njia nzuri za kuhimiza watu kujisomea vitabu. Tukiangalia hali ya usomaji vitabu katika nchi zetu za Afrika Mashariki naweza kusema hali si ya kufurahisha sana, inaonekana kuwa sisi watu wa Afrika Mashariki huwa tunapekua vitabu tunapokuwa shule na baada ya shule basi vitabu tunaweza pembeni. Hebu tumsikilize ofisa wa wizara ya elimu ya Kenya akieleza hali za usomaji wa vitabu nchini Kenya

    Fadhili: Naona sio wakati wa shule tu, hata tunapokuwa shule tunasoma vitabu wakati wa mitihani, baada ya mitihani vitabu tunaweka pembeni. Pili: Msemo husema vitabu huleta maendeleo ya binadamu. Kwa hiyo wasikilizaji, chukua kitabu chochote unachopata, tuanze mara moja kusoma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako