• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema marufuku iliyowekwa kwa ajili ya kuimarisha usalama katika eneo la Mpeketoni itaendelea kuwepo

    (GMT+08:00) 2015-03-26 15:48:15

    Naibu Gavana wa kaunti ya Lamu Eric Mugo na mbunge wa Lamu magharibi Julius Ndegwa hawakuridhishwa na uamuzi huo.

    Eric Mugo ameitaka serikali kuondoa marufuku hiyo akisisitiza kwamba maafisa wa usalama wamefanikiwa kuregesha usalama katika hali ya kawaida eneo hilo.

    Kiongozi huyo amesema viongozi hawawezi kuendelea kuwaruhusu raia waishi chini ya vikwazo hivyo kwani vinawalemaza kiuchumi.

    Inadaiwa kuwa maafisa wa polisi sasa wamekuwa kero kwa raia wa kaunti hiyo kwa kuwatia mbaroni mara kwa mara wanapofanya biashara nyakati za usiku.

    Joseph Nkaisery waziri wa Usalama alitakiwa kutoa mweleko mpya kuhusiana na kumalizwa kabisa kwa marufuku hiyo jambo ambalo hadi sasa limesalia kuwa ndoto ya mchana kwa wakaazi.

    Nkaisery aliidhinisha shuhuli za kawaida kuendelea katika kisiwa cha Lamu pekee na kuendeleza marufuku katika maeneo mengine kama Mpeketoni.

    "Vita vya usalama si va serikali ama waziri pekee ni jukumu la kila mmoja,tunatakiwa kushirikiana kuregesha hali ya kawaida."

    Hii ni baada ya mashambulizi ya kigaidi ya mwaka jana yalio sababisha vifo vya watu wasiokua na hatia zaidi ya mia 1.

    Mjadala wa viongozi wa Lamu ulifikishwa katika mikutano ya hadhara wikendi hii huku baadhi ya viongozi wakiunga mkono msako huo kuendelea kwa ajili ya usalama.

    Baadhi yao kama wawakilishi wa wodi wamesema usalama wa kitaifa unasalia kuwa suala muhimu sana katika jamii ya wakenya .

    Msako huo ukiendele unaweza kuwatia hofu wakaazi wanaotoka katika maeneo tofauti.

    Njomo Maina wa Bahari ametaka msako uendelee licha ya kuathiri biashara kwani usalama ni bora.

    Viongozi hao wanahoji kuwa marufuku hayo yamesaidia kuangamiza kabisa visa vya mashambulizi ya kigaidi Lamu kwani havivashuhudiwa tena.

    Katika maelezo yake ya mwisho mwezi Februari waziri wa usalama wa kitaifa alitangaza kwamba maeneo yalio karibu na mpeketoni yataendelea n marufu ya shuhuli za usiku ikiwemo ibada na biashara.

    Aliahidi kuondoa marufuku hayoo Mpeketoni lakini hajatoa amri hiyo hadi sasa.

    Hali hiyo imekuwa pigo kubwa kwa wafanyibiashara wanaotegemea jua la mchana pekee kufanyia kazi zao na kupata kipato.

    "Mimi ni Aboud Ali ,mfanyibiashara na mkulima ,natoka eneo la Kiwaiu nafanya biashara ya mikoko,kilimo na biashara zinazotumia usafiri wa baharini.

    Bahari ndio tegemeo letu kuu sasa tumekuwa kama panya tukifika jioni tunaamrishwa kuingia ndani ya nyumba tutulie.

    Sasa hatuwezi kufanya kazi yoyote wakati wa usiku na tunafanya mambo yetu sana usiku."

    Kwa wavuvi wa maeneo yote ya kaunti ya Lamu na usafiri wa baharini shuhuli hizo zimeendelea kuwa marufuku usiku.

    Mapema mwaka huu katika mahojiano na naibu naibu mwenyekiti wa Chama cha utalii kaunti ya Lamu Ghalib Ahmed Alwi alieleza namna marufuku hiyo ilivoathiri na kuleta hasara kubwa katika sekta ya utalii.

    Katika kisiwa kikuu cha Lamu ,wafanyibiashara walio na stakabadhi maalum pekee kutoka kwa idara ya usalama ndio wanaoruhusiwa kufanya kazi usiku.

    Hii ni mara ya tano kuahirishwa mda wa kusitishwa kwa marufuku hayo yalioanzishwa julai mwaka 2014.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako