• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AIIB kuongeza kasi ya uwekezaji barani Afrika

    (GMT+08:00) 2015-03-26 18:14:52

    Wachambuzi wanasema, maandalizi yanayoendelea ya kuzindua Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB yatabadili zaidi mazingira ya uwekezaji barani Afrika, na kusababisha kupungua kwa gharama huku yakiongeza ushindani katika soko la fedha la kimataifa.

    Gerishon Ikiara, mkurugenzi mshiriki katika kitivo cha Diplomasia na masuala ya Kimataifa kwenye chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya anasema, kuanzishwa kwa AIIB kutainua sura ya China kama nguvu inayoongoza katika mwenendo wa uwekezaji na kutoa mikopo duniani katika karne ya 21. Pia itaongeza upatikanaji wa rasilimali za uwekezaji duniani na kuinua ngazi ya ushindani katika soko la fedha la kimataifa. Ikiara anasema, rasilimali hizo zitaongeza ngazi ya ushindani katika soko la fedha la kimataifa na kupunguza ukiritimba ambao nchi za Magharibi zimekuwa nao katika siku zilizopita. Mkurugenzi huyo anasema, AIIB itaongeza kasi ya maendeleo ya miundombinu na uwekezaji barani Afrika na katika nchi nyingine zinazoendelea.

    China inaongoza katika juhudi za kuhakikisha kuwa Benki hiyo ambayo imeanzishwa kunatokana na pendekezo la China, inazinduliwa, na mpaka sasa, nchi 21 zimeshasaini Makubaliano ya Awali yanayounga mkono kuanzishwa kwa Benki hiyo. Nchi za Afrika zina fursa ndogo ya kupata ufadhili wa muda mrefu wa miradi ya miundombinu kutokana na mitaji isiyoridhisha na soko la fedha. Kuna mikataba mibovu ya miundombinu inayotolewa na nchi za Afrika kutokana na kile ambacho wataalam wa Benki ya Dunia wanasema ni uelewa mdogo wa ujuzi wa kibenki katika uwekezaji.

    Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia inatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi mwishoni mwa mwaka huu, ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani bilioni 50. Nchi 27, zikiwemo Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, na Italia, zimeonesha nia ya kujiunga na bodi ya Benki hiyo kama wanachama waanzilishi.

    Ikiara anasema, utayari na nia ya nchi muhimu za Ulaya kuunga mkono uanzishwaji wa Benki hiyo ni ishara kuwa, nchi za Ulaya zinatambua kuwa nafasi inayokua ya China katika sekta mbalimbali za uchumi wa dunia haiwezi kupuuzwa wala kuzuiwa. Kwa upande wa Afrika, Benki hiyo inachukuliwa kama suluhisho muhimu la mazingira ya kifedha ambayo zamani kwa kiasi kikubwa vilitawaliwa na misaada kutoka nje, pia ni maendeleo makubwa katika kuongeza fursa za kuchagua rasilimali za fedha. Nchi nyingi za Afrika zimefaidika na mikopo kutoka Benki ya China ya Wxim, na Benki hiyo mpya ni habari njema zaidi kwa nchi hizo.

    Nchi za Afrika Mashariki zinatekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuongeza uzalishaji wa umeme na upatikanaji wake nje ya mipaka yake, na pia zinawekeza katika nishati mpya. Ikiara anasema, AIIB inatarajiwa kuongeza kasi ya mchakato huo kwa kupanua na kufanya uwekezaji wa kisasa kwenye maeneo mbalimbali, uwekezaji wa jumla, na fursa za kibiashara.

    Amesema kutokana na nchi nyingi zinazotaka kujiunga na Benki hiyo, nchi mbalimbali duniani zitanufaika na mikopo mikubwa ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu, ikiwa ni matokeo ya kiasi kidogo cha riba ya mkopo katika miradi ya ujenzi wa miundombinu itakayotozwa na Benki hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako