• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Saudi Arabia na nchi nyingine zafanya tena mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa kundi la Houthi nchini Yemen

    (GMT+08:00) 2015-03-27 19:52:07

    Saudi Arabia na nchi nyingine zimefanya mashambulizi ya anga tena leo alfajiri kwenye maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa kundi la Houthi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa na mkoa wa kusini wa Taiz.

    Ofisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema, mashambulizi hayo yameharibu kambi mbili na kituo kimoja cha kurushia kombora kilichodhibitiwa na wapiganaji wa Houthi.

    Kutokana na ombi la rais Abd-Rabbu Mansour Hadi wa Yemen, Saudi Arabia na nchi nyingine za Ghuba zilianza mashambulizi hayo jana usiku katika mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa na miji mingine. Mbali na kuharibu vifaa vya kijeshi vilivyodhibitiwa na kundi la Houthi, mashambulizi hayo pia yamesababisha vifo vya raia 25 wa kawaida na wengine wengi kujeruhiwa.

    Kiongozi wa kundi la Houthi Bw. Abdul Malik Houthi amesema mashambulizi hayo yamekwenda kinyume na sheria za kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako