• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa wito kwa Asia kuvumbua mawazo mapya ya usalama

    (GMT+08:00) 2015-03-28 13:00:15
    Baraza la Asia limefunguliwa leo asubuhi huko Boao, mkoani Hainan kusini mwa China, ambapo rais Xi Jinping wa China akifungua mkutano wa mwaka wa baraza hilo, alitoa wito kwa nchi za Asia kuondokana na fikra za vita vya baridi na kuvumbua mawazo mapya ya usalama, akisema nchi za Asia zinapaswa kuwa pamoja katika kujitafutia namna ya kujenga usalama, kunufaik na usalama na kupata maendeleo.

    Rais Xi akifafanua alisema katika dunia ya hivi leo usalama unahusisha mambo mengi, na hakuna nchi moja inayoweza kujilinda usalama bila kuwepo kwa usalama duniani. Alisisitiza kuwa, nchi moja moja ina haki ya kushiriki kwa usawa kwenye mambo ya usalama ya kanda yake, pia ina wajibu wa kulinda usalama wa kanda hiyo, na ufuatiliaji wa haki wa kila nchi unapaswa kuheshimiwa na kuhakikishwa.

    Kuhusu pendekezo alilotoa la kuanzisha Ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri na Njia ya hariri baharini ya karne 21, rais Xi alisema hilo si kauli mbiu tu, bali ni hatua halisi. Nchi zaidi ya 60 zinazohusika zimeeleza matakwa ya kushiriki kwenye shughuli hizo, na waraka husika unaobaini malengo na maelekezo ya vitendo ya pendekezo hilo tayari umetungwa.

    Mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia utakaoendelea hadi kesho umewashirikisha watu mashuhuri 1,700 Asia na mabara mengine duniani, wakiwemo viongozi kutoka nje ya Asia, kama vile marais wa Amenia, Nepal, Indonesia, Sri Lanka, na rais Yoweri Musevini wa Uganda, marais kutoka Zambia na Austria, na viongozi wa serikali za Australia, Uholanzi, Sweden na Russia, ambao watajadiliana mambo yanayohusu uchumi, uslama, uvumbuzi wa teknolojia na huduma za jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako