• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa wito kwa Asia kuvumbua mawazo mapya ya usalama

    (GMT+08:00) 2015-03-28 20:10:38
    Baraza la Asia limefunguliwa leo asubuhi huko Boao, mkoani Hainan kusini mwa China. Rais Xi Jinping wa China akifungua mkutano wa mwaka wa baraza hilo, alitoa wito kwa nchi za Asia kuondokana na fikra za vita vya baridi na kuvumbua mawazo mapya ya usalama. Aidha, amesema kuwa, katika miaka mitano inajayo, China itaagiza bidhaa za dola trilioni 10 za kimarekani kutoka nje.

    Akizungumzia usalama wa barani Asia, rais Xi Jinping wa China amesema nchi za bara hilo Asia zinapaswa kuwa pamoja katika kujitafutia namna ya kujenga usalama, kunufaika na usalama na kupata maendeleo.

    Amesema katika dunia ya hivi leo usalama unahusisha mambo mengi, na hakuna nchi moja inayoweza kujilinda vizuri bila kuwepo kwa usalama duniani. Amesisitiza kuwa, nchi moja moja ina haki ya kushiriki kwa usawa kwenye mambo ya usalama ya kanda yake, pia ina wajibu wa kulinda usalama wa kanda hiyo, na ufuatiliaji wa haki wa kila nchi kuhusu suala la usalama unapaswa kuheshimiwa na kulindwa.

    Kuhusu pendekezo alilotoa la kuanzisha Ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri na Njia ya hariri baharini ya karne 21, rais Xi amesema zaidi ya nchi 60 zinazohusika zimeeleza nia ya kushiriki kwenye shughuli hizo, na waraka husika unaobaini malengo na utekelezaji wa pendekezo hilo tayari umetungwa.

    Akizungumzia maendeleo ya China katika siku za baadaye, Rais Xi amesema China haitayumba hata kidogo katika njia yake ya kujiendeleza kwa amani, mtazamo wake wa kutafuta maendeleo ya pamoja, na sera yake ya kuhimiza maendeleo kwa njia ya ushirikiano wa kikanda wa Asia Pasifiki.

    Amesema maendeleo ya uchumi wa China yataendelea kutoa fursa za biashara, uwekezaji na ushirikiano kwa nchi nyingine barani Asia na za mabara mengine, na kudokeza kuwa katika miaka mitano ijayo, China itaagiza bidhaa za zaidi ya dola trilioni 10 za kimarekani kutoka nje, huku thamani ya uwekezaji utakaofanywa na China katika nchi za nje kwa miaka mitano ijayo itazidi ikizidi dola bilioni 500 za kimarekani.

    Mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia utakaoendelea hadi kesho umewashirikisha watu mashuhuri 1,700 kutoka Asia na mabara mengine duniani, wakiwemo wakuu wa nchi, wakiwemo marais marais wa Amenia, Nepal, Indonesia, Sri Lanka, Austria pamoja na rais Yoweri Musevini wa Uganda na rais Edgar Lungu wa Zambia. Washiriki hao watajadili mambo yanayohusu uchumi, uslama, uvumbuzi wa teknolojia na huduma za jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako