• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazitaka nchi mbalimbali kupambana na ugaidi nchini Libya

    (GMT+08:00) 2015-03-28 20:17:15

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka nchi wanachama kupambana na ugaidi nchini Libya na kurefusha muda wa tume ya Umoja huo nchini humo hadi Septemba 15 mwaka huu.

    Katika azimio lililofikiwa na pande zote, baraza hilo limezitaka nchi wanachama kuchukua hatua zote kupambana na vitendo vya ugaidi, vikiwemo vile vya kundi la IS, makundi ya kigaidi yanayoapa kutii kundi la IS, kundi la Ansar al-Sharia na mtu yeyeote anayeshirikiana na kundi la al-Qaida nchini Libya.

    Baraza hilo lilieleza wasiwasi mkubwa juu ya athari mbaya zinazoletwa na makundi hayo nchini Libya na katika ukanda huo, na kusisitiza kuwa kuna haja ya kuchukua hatua ya pande zote dhidi ya makundi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako