• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko wa bomu huku Uchaguzi ukiendelea Nigeria

    (GMT+08:00) 2015-03-28 21:04:30

    Mlipuko umetokea kwenye kituo cha kupigia kura kusini mashariki mwa Nigeria katika jimbo la Enugu licha ya kwamba usalama umeimarishwa nchini humo wakati wa zoezi la upigaji kura wa uchaguzi mkuu nchini humo.

    Afisa mku wa polisi kwenye eneo hilo Dan Bature amesema bomu lilikuwa limefichwa chini ya gari moja katika shule ya WTC lakini mabomu mengine matatu yaliokuwa yamefichwa yameteguliwa na polisi wa kushughulikia vilipuzi.

    Kulingana na Tume huru ya uchanguzi nchini humo kuna wagombea 14 wanaouwania kiti cha urais lakini kinyang'ayiro kikali kitakuwa kati ya Rais wa sasa GoodLuck Jonathan na kiongozi mkuu wa upinzani jenerali Muhammadu Buhari.

    Lakini wakati huo huo tume hiyo ya uchaguzi imetangaza kuhahirishwa kwa kura ya wabunge katika jimbo la Jigawa kaskazini mwa nchi hiyo kutokana na uhaba wa makaratasi ya kupigia kura.

    Tume hiyo haikutangaza siku mpya ya uchaguzi.

    Waziri wa usalama nchini humo kanali Austin Akobundu amewahakikishia raia utulivu wakati wa zoezi hilo hasa kwenye maeneo ya kaskazini ambako hofu ya mashambuzli ya kundi la Boko Haram ilisababisha uchaguzi mkuu kuharishwa kwa wiki sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako