• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka wa malengo na utekelezaji wa mpango wake wa "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21"

    (GMT+08:00) 2015-03-28 21:20:32

    China imetoa waraka unaobainisha malengo na mpango wa utekelezaji wa mpango wake wa "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21".

    Waraka huo umeweka bayana kanuni, mwongozo, vipaumbele vya ushirikiano pamoja na taratibu za ushirikiano wa mpango huo uliopedekezwa na rais Xi Jinping wa China mwaka 2013.

    Lengo la mpango huo ni kuhimiza mtiririko huru wa mitaji, nguvu kazi na bidhaa, kugawa kwa ufanisi rasilimali, na mfungamano zaidi wa masoko kwa kuimarisha mwingiliano kati ya mabara ya Asia, Ulaya, na Afrika na bahari zilizo kati yao.

    Waraka huo umesema ujenzi wa miundo mbinu, biashara, ukusanyaji na mtiririko wa fedha ni miongoni mwa maeneo yanayopewa kipaumbele katika ushirikiano. Waraka huo unasisitiza kuwa utakelezaji wa mpango wa "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21" ni mchakato ulio wazi na wenye unyumbufu na unaoshirikisha pande mbalimbali.

    Waraka huo umetolewa siku tatu kabla ya siku ya mwisho iliyopangwa ya kuomba kujiunga na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, AIIB. Benki hiyo imeanzishwa kufuatia pendekezo laChina kwa ajili ya kutoa ufadhili wa fedha katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako