• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • 25 wauwawa katika shambulizi la Boko Haram nchini Nigeria mnamo siku ya uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2015-03-29 19:46:08

    Watu 25 wameuwawa na wengine 5 kujeruhiwa kwenye shambulizi lililotekelezwa na kundi la Boko Haram nchini Nigeria katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno huku nchi hiyo ikiendelea na zoezi la upigaji kura wa uchaguzi wa rais na wabunge.

    Gavana wa jimbo hilo Kashim Shettima anasema alipokea ripoti kuhusu shambulizi hilo leo asubuhi akikitaja kitendo hicho kuwa cha kikatili.

    Zaidi ya wapiga kura milioni 56 wamejitokeza kushiriki zoezi hilo. Kuna wagombea 14 wanaouwania kiti cha urais lakini kinyang'ayiro kikali kitakuwa kati ya Rais wa sasa GoodLuck Jonathan na kiongozi mkuu wa upinzani jenerali Muhammadu Buhari. Milolongo mirefu imekuwa ikishudiwa katika maeneo mbalimbali kote nchini humo huku polisi wakiimarisha doria.

    Hata hivyo shughuli za upigaji kura zimerefushwa hadi leo kutokana na hitilafu za mitambo ya kielektroniki ya kuthibitisha wapiga kura waliosajiliwa.

    Tume huru ya uchaguzi nchini humo imeawashauri maafisa wake wote walioko kweny zaidi ya vituo 300 vilivyoathrika kuendelea na shuhughuli hiyo jumapili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako