• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashambulizi ya angani mjini Sanaa yaingia siku ya nne

    (GMT+08:00) 2015-03-29 20:03:11

    Mashambulizi ya angani yanayofanywa na Saudi Arabia na nchi nyingi za Ghuba dhidi ya kundi la Houthu nchini Yemen jana yaliingia siku ya nne katika mji mkuu Sanaa.

    Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa askari kadhaa waliuawa katika mashambulizi jana usiku, lakini kundi la Houthi limekataa kutoa idadi ya watu waliouawa.

    Viongozi wa nchi za Kiarabu waliohudhuria mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu huko Sharm el-Sheikh nchini Misri, wametoa taarifa wakitaka wapiganaji wa Houthi waondoke mara moja nchini Yemen, hasa kwenye ofisi mbalimbali za kiserikali na kusalimisha silaha kwa mamlaka halali ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako