• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za kiarabu wakubali kuunda jeshi la pamoja

    (GMT+08:00) 2015-03-29 20:32:54

    Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misiri leo amesema nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zimekubali kuanzisha jeshi la pamoja kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka vya kiusalama.

    Akihutubia mkutano wa wakuu wa nchi za Kiarabu, rais Sisi amesema kamati ya ngazi ya juu itaundwa kutekeleza uamuzi huo, na viongozi wa majeshi ya nchi za kiarabu watafanya mkutano kujadili utaratibu husika wa jeshi hilo.

    Taarifa ya mwisho iliyotolewa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu kwenye mkutano huo inasema jeshi la pamoja litaingilia kwa njia ya kijeshi kukabiliana na vitishio vya amani na kiusalama katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kwa kufuati ombi la nchi husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako