• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usimamizi wa fedha za familia hapa China

    (GMT+08:00) 2015-04-09 13:04:01

    Katika utamaduni wa China wanaume na wanawake wanashirikiana kusimamia mali za familia, lakini kuna wakati wanawake wanasimamia matumizi ya kila siku ya fedha za familia, na wakati mwingine wanaweka kumbukumbu ya matumizi ya fedha ambayo wakati fulani wanaume wanaweza kuona ni madogo madogo na yasiyo na umuhimu mkubwa. Kutokana na sababu hii wasichana wa China toka wanapokuwa watoto wanafundishwa kusimamia fedha za familia. Na uhodari wao katika hilo, ni moja ya msingi wa hali bora ya familia. Jukumu kubwa la wanaume ni kufanya kazi ya kuchuma pesa.  Siku hizi tukio moja lilitokea mkoa wa Zhejiang Kusini mwa China, ambako jamaa mmoja wa mji wa Hanghzou aliadhibiwa na mkewe, baada ya mkewe kukuta hela kwenye mfuko wa suruali yake wakati anaenda kufua, lakini hakujua zimefikaje mfukoni. Mkewe alikasirika na kuandika bango na kumwambia aende nje akiwa amelivaa shingoni na maneno "mke wangu mpenzi na mzuri sana, najua nimefanya kosa, kuanzia leo nitakabidhi mshahara wangu wote kwako". Huyu jamaa alivalishwa bango hilo huku akiwa kifua wazi na kupiga magoti nje, tena wakati huo kulikuwa na baridi kiasi. Jamaa alikubali adhabu kwa sababu alikiuka utaratibu waliokubaliana na mkewe. Lakini isieleweke vibaya kuwa wanaume waliooa hapa China hawatakiwi kuwa na pesa mfukoni. Wanakuwa na pesa, lakini kilichopo ni kuwa matumizi ya pesa yanapangwa pamoja.

    Je, wanaume na wanawake wa China wana maoni gani kuhusu nani anadhibiti pesa nyumbani? Kwa undani zaidi hebu sikilize kipindi chetu.

     


    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako