• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maendeleo yaliyopatikana katika mambo ya wanawake nchini China na katika nchi za Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2015-04-09 19:57:19
    Hadi mwaka 2014, idadi ya jumla ya wafanyakazi wa kike imefikia milioni 137, kiasi hicho kinachukua asilimia 40 ya idadi ya jumla ya wafanyakazi nchini China. Mbali na hayo, kiwango cha elimu cha wanawake pia kimeinuka kwa udhahiri. Kwa mfano idadi ya wafanyakazi wanawake waliopata elimu ya chuo kikuu inachukua asilimia 51.9 ya idadi ya jumla ya wafanyakazi, kiasi hicho kimeongezeka kwa asilimia 34.6 kuliko miaka mitano iliyopita.

    Idadi ya wanawake wanaoshughulikia mambo ya utengenezaji, elimu, kilimo, misitu ufugaji na uvuvi, pamoja na software inaongezeka kwa asilimia 8.4, 1.9, 1.6, na 1.3, lakini pia idadi ya wanawake wanaoshika wadhifa wa uongozi katika sekta mbalimbali pia imeongezeka kwa asilimia 2.6 kuliko mwaka 2007. Ripoti ya uchunguzi kuhusu hali ya kulinda haki ya wafanyakazi wa kike imeonesha kuwa, haki ya ajira ya wafanyakazi wa kike imezidi kuhakikishwa, ambapo asilimia 67.8 ya wafanyakazi wa kike wanaridhika na hali ya kazi yao kwa hivi sasa, huku asilimia 50.9 wakiwa na wasiwasi kuhusu kupoteza ajira, na kiasi hicho kiko chini kwa asilimia 4.9 kuliko wafanyakazi wa kiume.

    Kiwango cha mapato ya wafanyakazi wa kike pia kimeinuka, na kufikia yuan 2403.8 kwa mwezi, sawa na dola za kimarekani 360 kwa mwezi, kiasi hicho kimeongezeka kwa asilimia 78.4 kuliko mwaka 2010. Haki za wanawake za kupewa huduma za jamii, haki za ajira, usalama na afya pia zinafuatiliwa zaidi. Hadi mwezi Septemba mwaka 2013, idadi ya vyama vya wanawake katika ngazi mbalimbali nchini China imefikia milioni 2.6. Mashirika hayo yamechukua hatua mbalimbali kulinda haki na maslahi za wafanyakazi wanawake kwa kufuata sheria.

    Kila mwaka Shirikisho la Wanawake la China linafanya tafrija ya wanawake wa China nan chi za nje ili kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Tafrija hiyo imefanyika tarehe 5 Mwezi Machi mjini Beijing. Katika tafrija hiyo, mwenyekiti wa Shirikisho la wanawake la China Bibi Shen Yueyue amekumbusha mafanikio yaliyopatikana katika maendeleo ya uchumi na jamii, pamoja na mambo ya wanawake ya China katika mwaka uliopita.

    Pia amesema mwaka jana Shirikisho la wanawake la China lilihimiza kuhusisha sheria ya kupambana na unyanyasaji wa kimabavu katika familia yenye mipango ya utungaji wa sheria katika halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China, kuhimiza kazi ya kuondoa ubaguzi wa jinsia katika mambo ya ajira, kutekeleza mipango ya utoaji wa mafunzo kwa wanawake, kusukuma mbele utoaji wa mikopo midogomidogo kwa wanawake, upimaji bure wa kansa ya matiti na kizazi kwa wanawake vijijini, kufanya kampeni ya kuondoa ugonjwa wa anemia kwa watoto wachanga, pamoja na miradi mingine inayowanufaisha wanawake na watoto.

    Si hayo tu, bali pia ameongeza kuwa, wanawake wa China wanapenda kushirikiana na wanawake wa nchi mbalimbali duniani na mashirika ya kimataifa kuhimiza usawa wa jinsia, kutimiza ukombozi na maendeleo ya wanawake, ili kuchangia zaidi katika kuhimiza amani ya kudumu na ustawi wa p amoja duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako