• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Daktari hodari wa China aliyetoa msaada nchini Zambia

    (GMT+08:00) 2015-04-17 15:15:22

    Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya China na Zambia, katika miaka ya 80 karne iliyopita, jeshi la ukombozi la umma la China lilianza kutoa msaada katika hospitali ya jeshi la Zambia bila ya sharti lolote. Kuanzia mwaka 1984 hadi leo, China imepeleka madaktari wapatao 200 wa makundi 18 kwenda nchini Zambia kutoa msaada wa matibabu. Kutoka Januari 21 mwaka 2013 hadi Januari 28 Mwaka 2014, Bw. Zhai Wenliang kutoka hospitali ya 175 ya jeshi la ukombozi la umma la China akiwa mkuu wa kundi la 16 aliongoza madaktari kumi na kufanikiwa kumaliza kazi ya kutoa msaada katika hospitali ya Maina Soko ya Zambia. Kazi yake ilisifiwa sana na wagonjwa wa Zambia pamoja na wachina wanaoishi nchini humo.











    Mwezi Oktoba mwaka 2012, hospitali ya 175 ya jeshi la China ilipewa kazi ya kutoa msaada nchini Zambia. Lakini katika wakati huo Bw. Zhai hakufahamu hali ya Zambia, alisikia tu kuwa Zambia ni nchi maskini iliyoko barani Afrika. Hata hivyo yeye ni mwanajeshi, kwani hakusita kuomba kubeba majukumu ya kwenda kutoa msaada nchini Zambia.



    "Kwa sababu mimi ni mwanajeshi, nina wajibu wa kuhudumia taifa, sisi wanajeshi tunatakiwa kujitolea. Pia nafikiri ninafaa kwa kazi hiyo, hivyo nilitoa ombi la kwenda Zambia."

    Zambia ambayo ipo kusini ya kati ya Afrika ni nchi inayokabiliwa na maambukizi ya malaria na Ukimwi. Nchi hiyo pia inakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya matibabu na dawa, idadi ya madaktari haizidi elfu moja kote nchini. Ili kuhakikisha kazi ya utoaji wa msaada inaendelea vizuri nchini Zambia, Bw. Zhai aliongoza madaktari wote kufanya maandalizi mara baada ya kukabidhiwa kazi hiyo. Bw. Zhai anasema,

    "Wakati ule naona mimi sikuwa daktari tu, bali ni mkuu wa kundi zima pia nilikuwa na wajibu wa kuwaongoza madaktari wengine. Hivyo nilituma barua pepe kwa ubalozi wa China nchini Zambia, na kuwasiliana na madaktari wa kundi la 15. Nafikiri kama tukiweza kuandaa vizuri zaidi, kazi hiyo itafanywa vizuri zaidi. "


    Ili kuweza kutimiza kazi ya utoaji wa msaada wa matibabu, la kwanza ni kujifunza lugha ya kigeni. Kabla ya kwenda nchini Zambia, Bw. Zhai alimwalika mwalimu wa kiingereza kutoa mafunzo ya lugha kwa madaktari wote. Baada ya kufika huko Lusaka, Bw. Zhai pia aliwaalika wafanyakazi wawili wa Zambia kuja kuzungumza nao, ili kuzoea lugha ya wenyeji wa huko na kuelewana vizuri na wagonjwa.

    Bw. Zhai alifahamu kuwa Zambia inakabiliwa na ukosefu wa dawa na madaktari, hivyo yeye na wenzake waliimarisha ujuzi wa matibabu na kuandaa dawa nyingi. Bw. Zhai aliwataka madaktari wote waweze kuwasaidia wengine kufanya upausaji. Baada ya kufika nchini humo, Bw. Zhai aligundua kuwa kutokana na hali duni ya matibabu, vifaa vya matibabu na dawa nyingi zilizotolewa na China nchini Zambia ziliachwa tu ghalani. Bw. Zhai aliwaongoza wenzake kuingia katika ghala kutafuta vifaa na dawa. Walikarabati vifaa vilivyoharibika, na kutafsiri kwa kiingereza majina ya dawa hizo.

    Mbali na hayo, Bw. Zhai aliwawekea madaktari malengo ya kikazi na kuleta ubunifu kwa huduma ya afya ya Zambia. Bibi Dou Yan ambaye ni mmoja wa kundi la 16 la madaktari anaona, malengo hayo yaliyowekwa na Bw. Zhai ni nguvu ya kuwachochea kufanikiwa kumaliza kazi ya utoaji msaada wa matibabu nchini Zambia.


    "Kama kusingekuwa na malengo aliyoyaweka, pengine tungefanya kazi ya kawaida tu ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa hospitali ya Maina Soko, kama tulivyofanya nchini China. Baada ya kuwa na malengo, tulitafuta Holter na kuwafundisha madaktari wa huko namna ya kuitumia. Pia tulifanikiwa kupima shinikizo la damu kwa mara kadhaa . "

    Maandalizi hayo yameleta mafanikio makubwa. Katika muda wa mwaka mmoja, ingawa kundi la 16 la madaktari wa China lilikabiliwa na hali duni ya vifaa vya matibabu, kukatika maji na umeme mara kwa mara , maambukizi ya malaria na UKIWI, lakini lilifanikiwa kuwatibu wagonjwa 6,000 hivi, na kupima wagonjwa mara 4,100. Wagonjwa wengi wa huko walisifia sana ustadi mzuri wa madaktari wa China na huduma nzuri walizozitoa. Mgonjwa mmoja wa kike aliyetibiwa na daktari wa China alielezea, ustadi mzuri wa daktari wa China.

    "Matibabu ni mazuri sana, najisikia vizuri sana. wakilinganishwa na madaktari wa Zambia, madaktari wa China wana ustadi mzuri zaidi. Najisikia vizuri, nashukuru matibabu ya madaktari wa China."

    Licha ya kutoa huduma ya matibabu, Bw. Zhai na wenzake pia walitumia teknolojia mpya kuanzisha huduma 15 mpya huko Lusaka. Mbali na hayo waliisaidia hospitali ya huko kuandaa madaktari. Kila daktari wa China aliwapatia mafunzo madaktari wawili hadi wanne wa Zambia.


    Sidnye Charlie alikuwa ni mmoja kati ya wasaidizi watano wa daktari wa Ultrasaundi wa China. Katika kazi ya kila siku, Charlie alijifunza ujuzi na uzoefu mwingi kutoka kwa daktari wa China. Kutokana na juhudi yake, Charlie alikuwa mkurugenzi wa ultrasaundi wa hospitali ya Mkoa wa Kaskazini ya Zambia. Kila anapozungumzia walimu wake wa China, hawezi kujizuia kuwasifu.

    "Madaktari wa China kweli ni walimu wazuri sana, walinifundisha mambo mengi. Nilidhani nafahamu mambo mengi, lakini ujuzi wa madaktari wa China unazidi sana ujuzi nilionao. "

    Muda ulikwenda haraka, Januari 27 mwaka 2014, kundi la 16 la madaktari wanaotoa msaada nchini Zambia walifanikiwa kumaliza majukumu yao na kurudi nchini China. Kwa ajili ya kupongeza kazi yao, wizara ya ulinzi ya Zambia iliwakabidhi madaktari hao "Medali ya Ushirikiano ya Kimataifa ya Mambo ya Ulinzi" ambayo ni alama ya urafiki kati ya China na Zambia.

    Baada ya kurudi nchini China, Bw. Zhai hakuweza kuisahau Zambia, anasema moyoni mwake Zambia ni kama nyumbani kwake kwa pili. Hadi leo, anaendelea kufuatilia hali ya Zambia, na kuwasiliana na madaktari na wagonjwa wa Hospitali ya Maina Soko kupitia Internet, pia kuwasalimia na wachina wanaoishi nchini Zambia kwa simu ya mikononi.

    "Kusema kweli, baada ya kurudi nchini China tuliiwazia sana Zambia. Tuliishi na kufanya kazi kwa mwaka mzima nchini Zambia, hivyo tunaipenda sana nchi hiyo. Nafikiri baada ya sisi kustaafu Tutakwenda tena Zambia kuangalia hospitali ambayo tuliifanyia kazi, na kuona jinsi hospitali hiyo inavyokuwa kutokana na msaada wa makundi ya madaktari wa China. Kama nikipata siku, nataka kurudi huko Zambia."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako