• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa afya za umma wa China Lu Hongzhou

    (GMT+08:00) 2015-04-17 15:28:03

    Mwaka jana ugonjwa wa Ebola ulilikumba eneo la Afrika Magharibi. Sierra Leone ikiwa ni moja ya nchi inayoathiriwa zaidi na ugonjwa huo, ilifuatiliwa sana na dunia nzima.

    Asubuhi ya tarehe 9 Novemba kikundi cha utoaji wa mafunzo ya afya ya umma kutoka China kikiwa na mtaalamu maarufu wa magonjwa ya kuambukiza Bw. Lu Hongzhou kilifunga safari na kwenda Sierra Leone.


    Kutokana na kuwa safari nyingi za ndege zinazoelekea katika nchi zilizokumbwa na ugonjwa wa Ebola kufutwa, kikundi hicho kiliwasili mjini Freetown nchini Sierra Leone baada ya saa 30.

    Freetown ulioko katika pwani ya bahari ya Atlantiki, ni bandari kuu na kituo cha biashara nchini humo, na moja kati ya sita ya watu wa nchi hiyo wanaishi kwenye mji huo. Wakati ugonjwa wa Ebola ulipoikumba Sierra Leone, utaratibu wa matibabu wa huko ulishindwa kabisa kuukabili na kuhitaji kuungwa mkono na kusaidiwa na nchi nyingine.

    Kutokana na takwimu zilizotolewa na shirika la afya duniani, hadi kufikia mwisho wa mwezi Oktoba mwaka 2014, watu zaidi ya elfu 13 walikuwa wameambukizwa virusi vya Ebola duniani, na watu elfu 5 hivi walikufa kutokana na ugonjwa huu. Wakati huo vikundi vingi vya utoaji wa msaada wa matibabu na mafunzo ya afya kutoka nchi mbalimbali na shirika la afya duniani vilikusanyika nchini Sierra Leone. Baada ya kuchambua hali halisi ya huko, wataalamu wa China waliamua kutoa mafunzo ya afya kwenye mitaa. Daktari Lu Hongzhou anasema,

    "Shirika la afya duniani linatoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi, na tuliamua kutoa mafunzo kwenye mitaa ambayo ni sehemu dhaifu. Kwani maambukizi ya ugonjwa ndani ya hospitali ni sehemu ndogo ya ueneaji wa ugonjwa huo, tunafanya juhudi ili kuzuia ugonjwa kuenea mitaani na kwenye mazishi. Kweli mafunzo tuliyotoa yalifanya kazi kubwa."

    Kutokana na mila za huko, kwenye mazishi watu hugusa mwili, lakini virusi vya Ebola vinaenea kwa maji ya mwili, hivyo zaidi ya nusu ya wagonjwa wa huko waliambukizwa kutokana na kugusa miili ya wagonjwa waliofariki. Bw. Lu amesema, mila za watu wa huko kuhusu kupuuza maambukizi ya Ebola ni sababu muhimu ya kutokea kwa hali mbaya ya maambukizi, na kutoa mafunzo kwenye mitaa kunaweza kuwaamsha watu wengi zaidi watilie maanani hali ya ugonjwa.

    "Tuliwahi kuona mgonjwa wa Ebola akifa wakati anatembea, na watu wengine wa huko walikuwa hawaogopi hata kidogo na kuendelea na shughuli zao wakipuuza ugonjwa huo. Hii inatokana na kukosa ujuzi kabisa wa ugonjwa huo. Tuliamua kutoa mafunzo kwa watu wa huko, tulitaka kuwafahamisha mwanzo wa ugonjwa huu, na namna ya kuepusha kuambukizwa, hivyo hatua za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo zinaweza kufanya kazi."

    Wataalamu wa China walianzisha darasa la kwanza la mafunzo ndani ya siku tatu. Daktari Lu Hongzhou na wataalamu wengine wa China walikwenda katika sehemu mbalimbali zilizokumbwa na ugonjwa wa Ebola, na kutafuta njia mwafaka zaidi ya kutoa mafunzo. Bw. Lu Hongzhou anasema,

    "Kwa mujibu wa upangaji wa majimbo ya uchaguzi nchini humo, tulitoa mafunzo moja baada ya lingine. Tulikuwa tunatoa mafunzo kwa maofisa wa huko, nao walikuwa wanawafahamisha watu wa kawaida, hivyo watu wote wanaweza kupata elimu ya kinga. Tulitoa mafunzo kwa lugha ya Krio, hivyo tuliweza kuwahamasisha watu wote. "

    Takwimu zinaonesha kuwa, ndani ya siku 65 tangu wataalamu wa China walipoanza kufanya kazi nchini Serra Leone, Bw. Lu Hongzhou na wenzake walitoa mafunzo kwa watu karibu elfu 3, ambao ni pamoja na maofisa wa mitaa na watu wanaofanya kazi mbalimbali ambao wanatoka miji na vijiji vilivyopo magharibi mwa Sierra Leone, sehemu iliyoathiriwa vibaya zaidi na Ebola. Na watu hao wamekuwa nguvu muhimu ya kukinga na kudhibiti ugonjwa wa Ebola.

    Kujikinga dhidi ya Ebola ni suala linalomkabili kila daktari anayefanya kazi katika eneo lenye maambukizi ya ugonjwa huo. Lakini wataalamu wa China wakivaa makazi maalumu ya kinga, itazuia mawasiliano na wenyeji waliopokea mafunzo. Daktari Lu alisema, pamoja na kufuata utararibu mkali wa usimamizi na kuua virusi mbalimbali, pia walijiandalia kukabiliana na hali mbaya.

    "Kila wiki tulipata habari ya daktari kuambukizwa, waliotoka Marekani, Shirika la afya duniani, Shirika la madaktari wasio na mipaka n.k., madaktari waliambukizwa na kufariki. Kwa hiyo nilipokwenda Afrika, sikuwaambia wazazi wangu, ili wasiwe na hofu. Pia nilipanga vizuri kazi nilizoacha. Nilifikiri kwa makini, kama niliambulizwa, basi ni hatma, nilijiandalia kukabiliana na hatari hiyo."

    Alipokuwa nchini Serra Leone, daktari Lu Hongzhou alibadilishana maoni na madaktari wa huko kuhusu matibabu, alialikwa kuhudhuria mkutano wa utafiti wa maambukizi mara mbili kila wiki, na kushiriki kwenye urekebishaji wa mwongozo wa matibabu.

    Alipozungumzia kutoa msaada nchini Serra Leone, Bw. Lu Hongzhou alisema alifanya uamuzi huu kwa sababu ni wajibu wa daktari.

    "Tunaishi pamoja dunia ambayo ni kama kijiji, hatupaswi kuona salama kutokana na tuko mbali na sehemu iliyokubwa na ugonjwa wa kuambukizwa. Hatuwezi kukaa kando wakati Afrika inapokumbwa na maambukizi ya ugonjwa."

    Mafunzo waliyotoa Bw. Lu Hongzhou na wenzake kwa madaktari wa mitaa, wahudumu wa afya za umma, maofisa wa mitaa na watu wanaojitolea kwenye mitaa, yamepata mafanikio makubwa na kupongezwa na serikali ya Serra Leone akiwemo rais wa nchi hiyo, na jumuiya za huko na za kimataifa. Mjumbe wa shirika la afya duniani nchini China Bw. Bernhard Schwartlander alipowasifu madaktari na wahudumu wa afya ya umma wa China alisema,

    "Watu hao waliondoka nyumbani na kusafiri mbali kwenda Afrika kupambana na ugonjwa wa Ebola. Kule hakuna hoteli nzuri wala familia yao, tena maisha ni magumu. Wao ni mashujaa halisi. Napenda kusisitiza kuwa, tunapaswa kutoa heshima na shukrani kwao."

    Wakati alipofanya majumuisho ya kazi ya kupambana na ugonjwa wa Ebola katika siku 65 nchini Serra Leone, daktari Lu Hongzhou alisema,

    "Tumejenga urafiki mkubwa na watu wa huko. Tunaona juhudi tulizofanya katika miezi hii miwili zina maana, na tumefanya tunachotakiwa kufanya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako