• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yeye ni mmoja wa madaktari wa kwanza wa China kutoa msaada Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2015-04-17 15:34:01

    Bw. Huang Fan ni daktari wa upasuaji katika hospitali ya Chuo kikuu cha udaktari cha Anhui, mashariki mwa China. Yeye pia ni baba wa watoto pacha. Alipokuwa na umri wa miaka 30, alijitolea kujiunga na wenzake wa kikundi cha kwanza cha kutoa msaada wa matibabu nchini Sudan Kusini. Yeye ni daktari mwenye umri mdogo zaidi katika kikuni hicho, na kujulikana nchini Sudan Kusini kama daktari anayeleta mwujiza.

    Sudan Kusini ilipata uhuru mwezi Julai mwaka 2011, na China ilipanga kutuma kikundi cha kwanza cha kutoa misaada ya matibabu nchini humo katika mwaka uliofuata. Daktari Huang alitoa uamuzi wa kushiriki kwenye kikundi hicho baada ya kufikiria kwa makini. Kuokoa maisha na kuwatibu wagonjwa ni wajibu wa kidaktari, lakini ilikuwa akienda Sudan Kusini, daktari Huang alipaswa kuagana na wazazi wake wenye umri mkubwa na hali mbaya ya afya pamoja na watoto pacha walio chini ya umri wa mwaka mmoja, na kumwachia mkewe kazi nzito ya kutunza familia kwa mwaka mmoja.


    Hata hivyo daktari Huang Fan aliamua kujiunga na kikundi cha kwanza cha madaktari waliokwenda kutoa msaada wa matibabu nchini Sudan Kusini. Alisema yeye bado ni kijana, na anahitaji kupata uzoefu na kujiendeleza kitaaluma katika kutekeleza jukumu hilo katika nchi za ng'ambo, na familia yake ilimuunga mkono.

    "Baba yangu alikuwa mwanajeshi, aliwahi kutumwa nje ya nchi kufanya kazi za kutoa msaada, kwa hiyo kutekeleza jukumu hilo ni kama urithi wa familia yetu. Binafsi naona hii ni fursa ya kupata uzoefu na ujuzi, hususan namna ya kutoa uamuzi katika wakati muhimu. "

    Mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka 2012, baada ya kuagana na familia yake, daktari Huang alifunga safari ya kwenda nchini Sudan Kusini. Kikundi chake kikiwa ni cha kwanza kupelekwa na China kutoa misaada ya matibabu nchini Sudan Kusini, kilikumbwa na shida nyingi zisizotarajiwa. Hapo awali madaktari wa Sudan Kusini na wenyeji hawakuwa na uelewa na imani na uwezo wa kikundi cha matibabu cha China, na pia kulikuwa na tatizo la mawasiliano, ilikuwa si rahisi kwao kuanza kufanya kazi kwa haraka. Bw Huang alisema

    "Mwanzoni ilikuwa vigumu kushirikiana na madaktari wenyeji. Tulikwenda na barua ya utambulisho kukutana na viongozi wa hospitali tukiongoza na wanadiplomasi wa ubalozi wa China nchini humo, kesho yake tukaanza kufanya kazi, madaktari na wauguzi wote wa pale walikuwa hawatufahamu kwa kuwa hakuna daktari hata mmoja wa China aliyewahi kwenda kwenye hospitali hiyo. Ilikuwa vigumu kwa makundi mawili ya wageni kushirikiana."

    Kwa hiyo Dt Huang Fan na wenzake walifanya karibu kila kitu, wakishiriki kwenye kazi ya kila siku ya kuwatembelea wagonjwa wanaolazwa hospitalini, kuwatibu wagonjwa wasiolazwa, kufanya upasuaji, hatua kwa hatua walianza kujenga urafiki wa kikazi na madaktari wenyeji. Na wakapokelewa kitaamuma na madaktari wenyeji baada ya kufanya kwa mafanikio upasuaji kadhaa mgumu sana.

    Mwezi Juni mwaka 2013, Bibi Agnes Dim aliyetoka kijiji cha maeneo ya Yeyi alikuwa na uvimbe ndani ya matiti wenye ukubwa kama mpira wa kikapu, na kuanza kubadilika kuwa kidonda. Madakari wa China hawasita kushughulikia suala hilo gumu, Daktari Huang na daktari mwenzake walifanya upasuaji kuondoa uvimbe huo. Upasuaji huo ulikuwa wa hatari kubwa, Dk Huang aligundua mishipa ya damu iliyolisha uvimbe ni vinene na kila mmoja ulikuwa na upana sawa na kidole cha mwisho, na kuzungusha uvimbe kunaweza kupasua mishipa ya damu na kusababisha damu kumwaga kwa wingi, hali ambayo inahatarisha masiha ya mgonjwa. Lakini kutokana na ustadi mzuri wa upasuaji, daktari Huang na mwenzake walishughulikia vizuri mishipa ya damu na kuondoa uvimbe kwa mafanikio.

    Kutokana na kufanya upasuaji kwa mafanikiwa mara kwa mara, madaktari waliondoa kabisa wasiwasi wa wenyeji kuhusu uwezo wao wa kitaaluma na kujenga umaarufu. Wagonjwa wengi walianza kuwafuata kwa ajili ya matibabu. Dk Huang alisema,

    "Tulikuwa na shinikizo kubwa la kufanya upasuaji katika nchi za nje kwa sababu sisi ni kikundi cha kwanza kupelekwa na China kutoa msaada wa matibabu katika nchi hii. Matatizo yakitokea yanatuathiri sisi binafsi, sifa ya China na hata uhusiano kati ya China na Sudan Kusini. Kabla ya kikundi chetu kuondoka, wagonjwa wote tuliowafanyia upasuaji, walipona. Naona kutoa msaada wa matibabu katika nchi za nje ni kazi tukufu, serikali yetu imefanya mengi kwa kufanikisha hazi hiyo na sisi madaktari tuliotekeleza jukumu hilo tunajisikia fahari kwa kutoa mchango wetu."

    Madaktari hao wa China wanaosifiwa na wenyeji kama madaktari walioleta mwujiza walifanya kazi huku wakiwa na hatari ya maisha yao. Walikuwa wanakabiliana na joto kali, hali duni ya kiuchumi, hatari ya kuambukizwa malaria na magonjwa mengine, na hata mabomu na risala.

    Tarehe15 Desemba mwaka 2013, siku chache tu kabla ya madaktari hao kurudi China, mgogoro wa kijeshi ulitokea katika mji mkuu Juba, ambapo matukio ya umwagaji damu yalisababisha vifo na majeruhi, na milio ya risasi kusikika mara kwa mara, hata tukio la kubadilishana risala kutokea ndani ya ua la makazi ya kikundi cha madaktari wa China. Daktari Huang na wenzake hawakubudi kujificha nyumbani na kuzuia milango na madirisha kwa samani, wakisikia milio ya risala nje ya nyumba. Pamoja na kujua kuwepo kwa hatari na wasiwasi mkubwa wa familia, kutojua vita itaisha lini wala wakati wa kurudi nyumbani, daktari Huang Fan na wenzake waliendelea na kazi yao na kufanikiwa kuwaokoa makumi ya wenyeji wa Sudan Kusini na wachina wanaoishi nchini humo. Waliporudi nyumbani, waziri wa afya wa Sudan Kusini Riak Gai Kok alitoa tuzo kwao na kuwasindikiza kutokana na mchango waliotoa, akiwasifu kuwa "mabalozi waliovaa nguo nyeupe" waliochangia urafiki wa Sudan Kusini na China. Daktari Huang Fan alisema

    "Ni lazima kikundi chetu cha madaktari kiwe mstari wa kwaza kufanya kazi. Hata wakati mapambano yalipolipuka, tulikwenda katika hospitali tuliyofanya kazi kuwakagua hali ya wagonjwa, watu wa Sudan Kusini watatukumbuka. Hii ni fahari yetu na hatutasahau kamwe. "

    Daktari huyo kijana Huang Fan, alisema pia amejifunza mengi alipokuwa nchini Sudan Kusini.

    "Leo naweza kusema bila kusita sijutii safari hiyo, hii ni faida kubwa kwa maisha yangu. Nilipita mambo mengi magumu na pia kujifunza mengi, nimenufaika sana kikazi na kimaisha. Nikipata nafasi napenda kurejea Sudan Kusini, pamoja na wenzangu walioshirikiana tutaendelea kuwahudumia watu wa Sudan Kusini."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako