• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya kutengeneza treni ya China CSR yawa "sura ya taifa" katika njia ya reli

    (GMT+08:00) 2015-04-29 14:25:53


     

    Utengenezaji wa kichwa cha treni cha umeme kilichobuniwa na kampuni ya kutengeneza treni ya China CSR kwa Afrika Kusini umekamilika katikati ya mwezi huu. Kichwa hicho cha treni ni aina ya 3 kusanifiwa na kampuni hiyo kwa mujibu wa hali halisi ya njia ya reli nchini Afrika Kusini katika miaka mitatu, na kabla ya hapo aina nyingine 2 za kichwa cha treni kinachoongozwa kwa nguvu ya umeme zilipewa jina la Mandela No.1 na Mandela No.2.

    Kwenye ukumbi wa makao makuu ya kampuni ya CSR hapa Beijing, sampuli za treni za kati ya miji na treni za mwendo kasi zinaonyeshwa kwa mpangilio mzuri. Kati ya sampuli hizo, inayovutia zaidi ni ya treni ya mwendo kasi aina ya CRH380A iliyobuniwa na kutengenezwa mwaka 2010. Treni hii imesifiwa kuwa ni kadi ya utambulisho ya treni za mwendo kasi za China, na mfano wa kuigwa wa uvumbuzi wa kujitegemea katika sekta ya utengenezaji wa vifaa.

    Mwenyekiti wa kampuni ya CSR Zheng Changhong anasema, "Treni hiyo ya mwendo kasi ni ya kasi zaidi duniani, ambayo inaweza kufikia kilomita 486.1 kwa saa katika hali ya majaribio. Kwa sasa, uwezo wa treni hiyo ni mzuri zaidi duniani, na unaendeshwa kwa utulivu. Treni hiyo ikiwa chapa ya China, imetambulishwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang kwa wakuu wa nchi nyingine."

    Mwaka 2011, treni hiyo ilipokimbia kwa majaribio kati ya miji ya Beijing na Shanghai, mwendo wake ulifikia kilomita 486.1 kwa saa, ambayo ilikuwa ni rekodi mpya ya mwendo wa treni duniani. Hivi sasa, treni hizo zinatumiwa kwa wingi katika safari kati ya Beijing na Guangzhou yenye umbali wa kilomita 2200, na inachukua saa 8 tu kusafiri kwa treni hizo.

    Baada ya treni ya mwendo kasi aina ya CRH 380A, kampuni ya CSR ilitumia miaka sita kutengeneza treni ya mwendo kasi ya ngazi tofauti kutoka kilomita 200 hadi 380 kwa saa.

    Kitu kinachostahili kutajwa ni kuwa juhudi za uvumbuzi zinazofanywa na kampuni ya CSR hazijawahi kusimama, na kwamba wamesanifu na kutengeneza treni ya mwendo kasi yenye kasi inayoweza kufikia kilomita 605 kwa saa katika hali ya majaribio, treni ya mwendo kasi inayoweza kuendeshwa katika baridi kali na upepo wenye mchanga, treni ya mwendo kasi ya sumaku ya kudumu, n.k. Msanifu mwandamizi wa kituo cha teknolojia cha Sifang kilicho chini ya kampuni ya CSR Cheng Jianfeng amesema uvumbuzi ni kiini cha chapa ya kampuni ya CSR, na ametolea mfano mchakato wa kusanifu treni ya mwendo kasi inayoweza kuendeshwa katika baridi kali na upepo wenye mchanga.

    "Treni hiyo inaweza kuvumilia halijoto kutoka nyuzi 40 chini ya sifuri hadi nyuzi 45. Kwa mujibu wa utafiti wetu, hali hiyo inatokea kila baada ya miaka 30 hadi 50, lakini ili kuthibitisha uwezo wa treni yetu wa kuvumilia joto na baridi kali, tulisanifu na kutengeneza treni mbili za sampuli na kuzisafirisha kwenye maabara iliyopo Austria na kufanya vipimo juu ya uwezo wa kiyoyozi, mfumo wa kuvuta behewa, mlango, waipa za kioo, n.k. Matokeo ni mazuri. Hivi sasa, treni hizo zinafanyiwa majaribio ya upepo mkubwa mjini Urumqi."

    Kutokana na uwezo mkubwa wa uvumbuzi wa teknolojia, nguvu ya ushindani ya kampuni ya CSR inazidi kuimarika. Mwenyekiti wa CSR Zheng Changhong anasema, "Kwanza, tuna uwezo mkubwa zaidi wa utengenezaji duniani, ambao ni treni 200 kwa mwaka, na tunahakikisha oda zinakamlika kwa wakati. Pili, tunaweza kuwasaidia wateja kupunguza gharama, ambazo ni za chini kwetu kuliko kampuni zote za nchi za nje. Tatu, China ina mtandao mkubwa zaidi wa treni za mwendo kasi, ambao unafikia kilomita elfu 16 ambayo ni nusu ya urefu wa njia ya treni za kasi duniani, na pia treni hizo zinaendeshwa katika hali mbalimbali, kutoka baridi kali hadi ukanda wa tropiki, kutoka sehemu za pwani hadi jangwa. Nne, aina za treni ni nyingi, zikiwemo kasi ya kilomita 140, 160, 200, 250, 300-350 na 380 kwa saa. Tano, kampuni ya CSR pia imesanifu treni ya majaribio ya mwendo kasi inayoweza kufikia kilomita 500 kwa saa, kufanya utafiti na majaribio kuhusu tekonolojia ya kisasa katika sekta ya treni ya mwendo kasi ili kutoa treni ya mwendo kasi ya kizazi kijacho."

    Katika kiwanda kimoja cha CSR, kuna karakana moja maarufu, ambayo waziri mkuu wa China Li Keqiang aliitembelea mwezi Julai mwaka jana. Hivi sasa, treni zaidi ya kumi zinaundwa kwa taratibu katika karakana hiyo. Ofisa wa kampuni hiyo Han Jun amesema treni hizo zitauzwa kwa nchi mbalimbali duniani.

    "Tumesanifu na kutengeneza treni kwa kufuata mahitaji tofauti ya wateja wetu. Treni zinazotengenezwa katika karakana hii zitauzwa kwa Malaysia, Singapore, Uturuki, Afrika Kusini, Ethiopia, na mwaka huu pia tutatengeneza treni kwa Macedonia."

    Han Jun amesema ushindani kwenye soko la kimataifa ni mkali sana, hata hivyo CSR inajitahidi kupata oda kutokana na ubora wa bidhaa. Mbali na hayo, CSR pia inatilia maanani mafungamano ya kitamaduni. Kwa mfano, kichwa cha treni kinachouzwa kwa Malaysia kimesanifiwa kwa umbo la kichwa cha Chui wa Malaysia, pia treni hiyo ina behewa maalumu kwa wanawake, pamoja na chumba cha kuswali kwa waislamu.

    Miaka 18 iliyopita CSR ilianza kusafirisha treni nje ya China, hivi sasa, bidhaa zake zimeuzwa kwa nchi na sehemu 84 duniani, na pia kampuni hiyo imejenga viwanda nchini Uturuki, Afrika Kusini, Malaysia na Argentina, kuwaajiri wafanyakazi wageni elfu 5, na kushiriki katika utungaji wa vigezo 59 vya kimataifa.

    Katibu mkuu wa chama cha kikomunisti katika kampuni tanzu ya Zhuji ya CSR Fu Chengjun amesema katika kushiriki ushindani katika soko la kimataifa, kampuni ya CSR imetimiza mabadiliko kutoka kuuza bidhaa tu hadi kutoa mipango kabambe ya ufumbuzi kwa wateja.

    "Tukitoka nje tunawakilisha sura ya kampuni za China, hivyo tunashikilia kanuni za uaminifu na kutimiza ahadi, na pia tunatetea wazo la mafanikio kwa pande zote mbili. Wateja wanaweza kuokoa pesa kwa kununua bidhaa na huduma zako, na pia wanapata huduma za kiwango cha juu, kama hatuna wazo hilo, biashara haitadumu kwa muda mrefu."

    Aidha, kampuni ya CSR inapanua soko la nje kwa njia ya matumizi ya mitaji kama vile kuunganisha au kununua kampuni nyingine. Hadi kufikia sasa, kampuni ya CSR imenunua kampuni sita katika nchi nne za Uingereza, Ujerumani, Australia na Singapore, fedha zilizotumiwa katika mchakato huo zimezidi dola za kimarekani milioni 640.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako