• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania aishukuru serikali ya China kwa kuzuia biashara haramu ya pembe za ndovu

    (GMT+08:00) 2015-04-30 18:59:45

    Waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania Mh. Lazaro Nyalandu amemwandikia barua balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing akitoa shukurani kwa serikali ya China kwa mchango wake katika kuzuia biashara haramu ya pembe za Ndovu na kulinda Ndovu.

    Katika barua hiyo, Nyalandu amezungumzia juhudi za serikali, vyombo vya habari, na wananchi wa China za kupunguza mahitaji ya pembe za Ndovu. Amesema takwimu zilizotolewa na shirika la kimataifa la kulinda wanyamapori WildAid zinaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wa China wameunga mkono kupiga marufuku biashara ya pembe za Ndovu, na katika kampeni nyingine dhidi ya matumizi ya mapezi ya papa, China imepata mafanikio makubwa kiasi kwamba mahitaji ya mapezi yamepungua kwa asilimia 50 hadi 70.

    Akikumbushia historia, Nyalandu amesema wakati biashara ya kimataifa ya pembe za Ndovu ilipopigwa marufuku mwaka 1989, uwindaji haramu ulipata pigo kubwa kutokana na kushuka kwa bei kwa asilimia 75, na idadi ya Tembo nchini Tanzania iliongezeka. Lakini kinachosikitisha ni kwamba ujangili ulianza kushamiri tena baada ya biashara hiyo kuruhusiwa tena mwaka 2008.

    Nyalandu pia amezungumzia juhudi za serikali ya Tanzania katika kuhifadhi tembo, akisema, serikali ya Tanzania inashirikiana na WildAid kama ilivyo serikali ya China, kuongeza ufahamu kwa wananchi kuhusu athari ya ujangili kwa kupitia vyombo vya habari na kuwashirikisha viongozi wa kidini. Anatarajia kuongeza ushirikiano na China katika kazi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako