• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema Marekani na Philippines kuimarisha ushirikiano wa kijeshi hakutasaidia amani na utulivu wa kikanda

    (GMT+08:00) 2015-05-01 10:12:42

    Msemaji wa wizara ya ulinzi wa China Bw. Geng Yansheng amesema, baadhi ya nchi zinaimarisha ushirikiano wa kijeshi, kufanya luteka kubwa ya pamoja na kuleta hali ya wasiwasi katika kanda ya Asia, hali ambayo haiendani na mwelekeo wa maendeleo ya amani na ushirikiano wa kunufaishana.

    Bw. Geng Yansheng aliyasema hayo kutokana na Marekani na Philippines zilifanya luteka ya pamoja kuanzia tarehe 20 hadi tarehe 30 Aprili.

    Bw. Geng pia ametangaza kuwa China na Russia zitafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi baharini katikati ya mwezi Mei. Amesema kuwa mazoezi hayo hayalengi nchi nyingine, na wala hayahusiani na hali ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako