• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu karibu 5,600 wafariki kutokana na tetemeko la ardhi Nepal

    (GMT+08:00) 2015-05-01 11:05:35

    Ofisi ya uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa mataifa, OCHA imesema idadi ya vifo vya watu kutokana na tetemeko la ardhi nchini Nepal imekaribia 5,600, na watu zaidi ya 11,100 wamejeruhiwa.

    Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, nyumba zaidi ya laki 1.3 zimebomoka na nyingine 86,000 zimeharibika. Pia amesema watu 24,000 wanakaa katika kambi 13 karibu na Kathmandu.

    OCHA pia imeripoti kuwa kutoweza kuzifikia baadhi ya sehemu zilizo mbali, ukosefu wa helikopta, hali mbaya ya mawasiliano na wasiwasi wa usalama, bado ni changamoto kubwa kwa kazi ya kusafirisha misaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako