• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazindua hatua za kuongeza soko la ajira

    (GMT+08:00) 2015-05-01 16:47:13

    Baraza la Serikali la China limetoa waraka unaoeleza hatua nne zinazoitaka serikali katika ngazi mbalimbali kurahisisha ujasiriliamali na uvumbuzi na kuunda nafasi zaidi za ajira.

    Hatua hizo ni pamoja na kuambatanisha sera za bajeti, kodi, fedha, biashara na sera ya ajira, kutoa kipaumbela kwa mradi unaoweza kutoa nafasi zaidi na nzuri za ajira wakati wa kuchagua miradi ya kuwekeza, kuzingatia umuhimu wa kampuni ndogo katika kutoa nafasi za ajira, na kurekebisha sera ya bima ya ukosefu wa ajira.

    Waraka huo umesema serikali inatakiwa kurekebisha sera zake na kuendelea kushawishi umma kuhusu ujasiriamali na kuanzisha biashara, ili kuchochea injini mpya ya ukuaji wa uchumi.

    China inakabiliwa na kazi ngumu ya kuhakikisha ajira kwa mwaka huu wakati ikikabiliwa na kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi.

    Serikali ya China imeahidi kuunda ajira zaidi ya milioni 10 sehemu za mijini na kuhakikisha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira hakiongezeki zaidi ya asilimia 4.5 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako