• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Maendeleo ya Rwanda (BRD yapeana mkopo kwa sekta binafsi

    (GMT+08:00) 2015-05-01 20:34:02

    Alex Kanyankole, afisa mtendaji mkuu, wa Benki ya Maendeleo ya Rwanda (BRD) anasema watapeana mikopo ya muda mrefu ya franc bilioni 68 kwa sekta binafsi mwaka huu.

    Kanyankole anaeleza benki hiyo imewacha huduma za amana na kutoa fedha kuzingatia kupeana mikopo kwa sekta muhimu za uchumi, kama vile kilimo, makazi ya gharama nafuu na nishati.

    Anasema, tofauti na benki za biashara, Benki ya Maendeleo ya Rwanda (BRD) itakopesha fedha kwa makampuni binafsi na miradi ambayo iko katika sekta za kipaumbele katika viwango cha bei nafuu kati ya asilimia 12 na 16 kwa mwaka.

    Kulingana na taarifa ya fedha ya mwaka wa 2014 ya benki hiyo, zaidi ya franc bilioni 93.6 ilipeanwa kwa miradi mbalimbali, huku faida ya mapato yake ilikuwa katika franc bilioni 10.12.

    Jumla ya mapato ya uendeshaji shughuli katika Benki hiyo, ilifikia franc bilioni 10.5, wakati gharama za uendeshaji wake ilisimamia franc bilioni 6.8 zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako