• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asisitiza ulazima wa kunufaika kwa watu waishio vijijini na matunda ya mageuzi

    (GMT+08:00) 2015-05-02 19:42:12

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kuendeleza kwa pamoja miji na vijiji na kuwashirikisha watu waishio vijijini katika mchakato wa mageuzi na maendeleo ili wanufaike nayo.

    Rais Xi amesema hayo alipoendesha mkutano wa ofisi ya siasa kuhusu utaratibu wa kuratibu maendeleo ya miji na vijiji.

    Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni serikali imeongeza sera za kuwawezesha wakulima, hadhi ya kilimo katika maendeleo ya taifa imeimarishwa na shughuli za kijamii vijijini zimeboreshwa, lakini miji na vijijini bado haijapata maendeleo ya uwiano. Amesema inapaswa kuzichukulia miji na vijiji kama kitu kimoja kitu kimoja wakati wa kupanga mikakati ya maendeleo na kugawanya raslimali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako