• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya wakimbizi 200, 000 wa Sudan Kusini wameingia Ethiopia tangu 2013

    (GMT+08:00) 2015-05-02 19:50:43

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema kuwa idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wamekimbilia Ethiopia tangu mapigano kuzuka nchini humo Desemba mwaka 2013 imefikia zaidi ya 200,000 .

    Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema wengi wanakimbia kutoka mapigano mapya katika majimbo ya Upper Nile na Jonglei au kama hatua ya tahadhari.

    Wafanyakazi wa UNHCR pia wameshuhudia ongezeko kubwa la wakimbizi wa Sudan Kusini kutoka watu 1,000 kwa mwezi katika robo ya kwanza ya mwaka huu hadi zaidi ya wakimbizi 4,000 waliosajiliwa mwezi Aprili.

    Umoja wa Mataifa kwa sasa unasajili zaidi ya wakimbizi 10,000 wapya katika vituo mbalimbali vya kuingia katika eneo la Gambella nchini Ethiopia.

    Waliofika wanaelezea kutembea kwa siku kadhaa kupitia kichaka wakiwa na chakula na maji kidogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako