• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Baltimore waendelea kurudi kwenye hali ya kawaida

    (GMT+08:00) 2015-05-02 20:20:38

    Mji wa Baltimore wa jimbo la Maryland nchini Marekani ulioshuhudia maandamamo ya vurugu ya zaidi ya wiki moja unaendelea kurudi kwenye hali ya kawaida baada ya maofisa 6 wa polisi wa mji huo waliohusika na kifo cha mtu mwenye asili ya Afrika kufunguliwa mashtaka ya uhalifu.

    Tangazo hilo lisilotegemewa lilitolewa na mwendesha mashitaka wa mji huo Marilyn Mosby likisema kijana huyo mweusi Freddie Gray alikuwa na majeraha mabaya kwenye shingo kutokana na kuwekwa pingu mikononi na miguuni ndani ya kituo cha polisi cha Baltimore.

    Tangazo hilo limewapa moyo watu mjini humo ambao wanaendelea kuandamana, wakiwa na tabasamu nyusoni kinyume na hapo nyuma.

    Hata hivyo, amri ya kutoruhusu kutembea usiku iliotolewa mjini humo tangu jumatatu iliyopita bado inaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako