• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujikinga kwa kutumia Wu Shu

    (GMT+08:00) 2015-05-04 15:35:40

    Mwezi Desemba mwaka 2012 dunia ilizizima kutokana na mwanamke mmoja kubakwa nchini India, ambapo baadae alifariki dunia. Kusema kweli tukio hilo lilihuzunisha wengi sana, sio nchini India pekee, bali nchi mbalimbali duniani, wanawake kwa wanaume waliandamana kupinga vitendo vya ubakaji, lakini kwa bahati mbaya, vitendo hivyo bado vinaendelea hata sasa. Nchini Afrika Kusini, mwanaume mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka 1,535 jela kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuwabaka wanawake 30 katika kipindi cha miaka mitano. Madhara yanayompata mwanamke alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili ni makubwa zaidi kimwili na kisaikolojia, na kuna wanawake wengine huamua kujiua kutokana na aibu pamoja na msongo wa mawazo.

    Sasa ili kukabiliana na hali hiyo, wanawake wameanza kujifunza Wu Shu, ili kuweza kujikinga dhidi ya vitendo vya ubakaji na vingine vinavyowadhalilisha. Mwanamke ni kiumbe dhaifu kuliko mwanamume, hivyo ni rahisi kuwa waathirika wa vitendo vyovyote vya kimabavu. Kwa kutambua hilo, mwanamke anaweza kupigana na mwanamume kwa kutumia kiwiko, goti, kiganja cha mkono, kufinya, au paji la uso, na kupiga kwa nguvu sehemu nyeti za mhalifu. Kiwiko, goti, kiganja, vidole, na paji la uso ni vidogo, ila vina uwezo mkubwa wa kuumiza, hivyo humsaidia mwanamke kutotumia nguvu nyingi.

    Tena kiwiko ni silaha kubwa sana, goti lina nguvu, kiganja ni chepesi, kidole ni kinaweza kutumika kwa njia nyingi. Unaweza kukunja ngumi kwa kutumia vidole, au hata kumtoboa macho mhalifu kwa kutumia vidole, tena tukizungumzia kicha, kichwa ni kigumu sana, na ukipata upenyo na kumpiga kisawasawa mhalifu, hakika ataumia. Mbinu hizi zinaweza kutumiwa kujilinda unapoona mazingira sio mazuri na kuna hatari ya kuvamiwa. Lakini pia, tukumbuke mwanamke ni kiumbe dhaifu, na anapovamiwa, woga unamwingia na hivyo kushindwa kujitetea.

    Inakuwa ngumu sana maana kuna mambo kadha wa kadha yanapita akilini mwako kwa sekunde chache, lakini, kama wakiweza kukabiliana na hali hiyo kwa utulivu na kutumia mbinu hizo, wana nafasi kubwa ya kuwashinda na hata kuwadhibiti wahalifu. Ila sasa, inapotokea wameshindwa kuwa watulivu na kukurupuka, hali hii inaweza kuwakasirisha hao wahalifu na matokeo yakawa mabaya zaidi.

    Ni kweli maana hao wahalifu watakuwa na hasira zaidi na kama waswahili wanavyosema, hasira zao watazimalizia kwa huyo mwanadada. Kule nchini Kenya, wanawake nao wamechoshwa na vitendo vya kudhalilishwa wanavyofanyiwa, kuna wakati wanawake walikuwa wakivuliwa nguo hadharani, kisa tu hawajajihifadhi vizuri. Kwa kuzingatia hilo, wanawake hao nao wameamua kujifunza Wu Shu ili kukabiliana na hali hiyo endapo itatokea.

    Serikali ya Kenya, polisi na wenyeji wakiendelea na harakati za kupunguza visa vya ubakaji katika sehemu mbali mbali nchini humo, kundi moja la kina mama katika kitongoji duni cha Koroghocho jijini Nairobi, limejipatia njia tofauti ya kujikinga kutokana na hatari hiyo ya ubakaji. Kina mama hao wamepokea mafunzo ya Wushu kutoka kwa shirika moja kwa jina No Means No, mafunzo ambayo kwa sasa wanayatumia kujikinga dhidi ya ubakaji katika kitongoji hicho.

        Pia kuna njia moja ambayo mwanamke anaweza kutumia kupambana na mbakaji au mhalifu. Nayo ni kumshambulia wakati ambao mhalifu hategemei. Watu kama hao wanaamini kuwa wanawake ni dhaifu na hajiwezi, hivyo ukimshambulia wakati hategemei, ni lazima atastuka, na mshtuo wake utampa nafasi mwanamke kutumia mbinu alizofundishwa kukabiliana naye.

    Mwanamume anapomvamia mwanamke, anajua kuwa ni kiumbe dhaifu, hivyo hachukui tahadhari yoyote ya kujikinga. Sasa mwanamke anapokuwa anavutwa au kukumbatiwa na mhalifu, hiyo inakuwa ni fursa nzuri kwake kufanya shambulizi la ghafla ambalo litamwezesha kumshinda na hata kumdhibiti mhalifu mpaka msaada utakapopatikana.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako