• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za China zajenga reli kwa makini kwenye Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2015-05-06 10:27:28








     

    Bandari ya Djibouti ni moja kati ya bandari kubwa katika nchi za Afrika Mashariki, ambayo iko kwenye sehemu muhimu kati ya Ghuba ya Aden na bahari nyekundu. Bidhaa nyingi zinazotoka na zinazokwenda jirani yake EthiopiaDjibouti zinapitia katika bandari hiyo. Barabara inayounganisha nchi hizo mbili haiwezi kukidhi mahitaji ya mawasiliano, na gharama za usafirishaji ni kubwa sana. Lakini hali hii itaboreshwa baada ya muda si mrefu, kutokana na ujenzi unaoendelea wa reli ya umeme kutoka Ethiopia hadi Djibouti. Hivi sasa ujenzi wa reli hiyo umefikia hatua za mwisho.

    Reli hiyo ya umeme inayounganisha Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia na mji wa Djibouti, ina urefu wa kilomita 740, ambayo inajengwa na kampuni za China. Mwendo wa treni kwenye reli hiyo utafikia kilomita 120 kwa saa. Uwekezaji mwenye mradi wa reli hiyo umefikia dola za kimarekani bilioni 4, na asilimia 70 ya uwekezaji imetolewa na benki ya Exim ya China. Mradi huo ulianza kujengwa mwezi Aprili mwaka 2012, na unatarajiwa kuzinduliwa mwezi Oktoba mwaka huu. Kampuni ya uhandisi na ujenzi iliyo chini ya kundi la ujenzi wa reli la China imebeba majukumu ya ujenzi wa reli kilomita 340 nchini Ethiopia na reli kilomita 100 nchini Djibouti.

    Msaidizi wa meneja mkuu wa kampuni ya uhandisi na ujenzi ya China ambaye ni mwakilishi mkuu wa kampuni hiyo barani Afrika Bw. Li Wuliang amesema, reli kutoka Ethiopia hadi Djibouti ni muhimu sana katika kutatua tatizo la usafirishaji la Ethiopia na kuhimiza mawasiliano ya kiuchumi na wananchi kati ya Ethiopia na Djibouti. Anasema,

    "Hivi sasa zaidi ya asilimia 90 ya bidhaa za Ethiopia zinasafirishwa kupitia bandari ya Djibouti. Baada ya kukamilika kwa reli hiyo, kusafirisha bidhaa kutoka Addis Ababa hadi bandari ya Djibouti kutachukua muda ndani ya saa 10 hadi 12, na urefu wa reli hiyo ni kilomita 700 zaidi, ambayo ni mfupi sana ikilinganishwa kusafirisha bidhaa barabarani. Tunakadiria kuwa gharama za usafirishaji kwa njia ya reli hiyo zitakuwa robo au moja tano ya gharama za usafirishaji kwa barabara. Baada ya kuzinduliwa kwa reli hiyo, inakadiriwa asilimia 70 ya usafirishaji utahamia kutoka barabara hadi reli hiyo. "

    Hali ya hewa ya Djibouti ni joto sana. Ingawa mwezi Aprili si mwezi ambapo hali ya hewa ni joto zaidi, lakini bado ni joto kali. Chini ya jua kali, wafanyakazi wa China walikuwa wanaweka mataluma ya reli huko Holhol, kilomita 40 nje ya mji waDjibouti, ambapo litatokeza daraja refu zaidi ya reli nchini humo. Waziri wa mawasiliano wa Djibouti Bw.Moussa Ahmed Hassan na meneja mkuu wa kampuni ya reli ya nchi hiyo walitembelea sehemu ya ujenzi, na kushuhudia uwekaji wa mataluma ya reli.

    Reli ya kipimo chembamba kutoka Ethiopia hadi Djibouti iliyojengwa na Ufaransa miaka 130 iliyopita, ni kama haiwezi kufanya kazi tena kutokana na kutoboreshwa na kutokarabatiwa kwa muda mrefu. Bw. Hassan amesema mradi wa ushirikiano wa reli hiyo ya umeme una maana muhimu. Anasema,

    "Reli hiyo mpya inayojengwa itaonesha umuhimu mkubwa katika maendeleo ya uchumi ya nchi yetu Djibouti na nchi nyingine ikiwemo Ethiopia. Tunaamini kuwa mradi huu utahimiza maendeleo ya uchumi wa Djbouti na kuongeza nafasi za ajira. China inatusaidia, na tunaheshimu sana uhusiano wa kiwenzi kati yetu na China."

     

    Kama waziri Hassan alivyosema ujenzi wa reli hiyo si kama tu utahimiza uchumi wa nchi za Ethiopia na Djibouti, bali pia umeongeza nafasi za ajira za huko. Bibi Saadya Otar mwenye umri wa miaka 32 aliyehitimu kutoka Chuo Kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing, hivi sasa anashughulikia kazi ya utafsiri kwenye sehemu ya ujenzi wa kituo cha treni karibu na mji wa Djibouti. Amesema wafanyakazi wenyeji wanaridhika na kazi na mapato yao.

    "Hapa kuna wafanyakazi 150, naona kazi zao ni nzuri na wanaridhikana na kiwango cha mapato. Kila siku wanajitahidi kufanya kazi, hivyo naona mradi huo utakamilishwa mapema."

    Kihalisi mawasiliano na ushirikiano kati ya wachina na wafanyakazi wenyeji zimepitia mchakato usio rahisi . Meneja wa mradi anayeshughulikia ujenzi wa reli sehemu ya Ali Sabieh anasema,

    "Mwanzoni nilipofanya mazungumzo na wafanyakazi wa huko, baadhi yao hawakunielewa na hata walinitupia mawe. Utamaduni wa kampuni yetu ni kuleta manufaa kwa raia wa huko, tumetoa mamia ya nafasi za ajira kwa huko, pia tumeboresha vifaa vingi vinavyohusiana na maisha ya raia mjini Ali Sabieh. Baada ya miezi mitatu na minne, wafanyakazi wenyeji wakaanza kutuelewa na kufanya kazi kwa jitihada."

    Reli hiyo kutoka Ethiopia hadi Djibouti ni reli ya kwanza ya kisasa inayopitia kwenye nchi mbili za Afrika Mashariki, pia ni reli ya umeme ya kwanza inayojengwa kwa mujibu wa vigezo vyote vya China. Kuanzia usanifu, ujenzi, usimamizi, hadi kipimo cha reli, mashine za ujenzi, ishara za mawasiliano, zana za umeme na kichwa cha treni, zote zimetumia teknolojia na bidhaa za China. Naibu meneja mkuu wa mradi wa reli hiyo Bw. Ding Zhaojun amesema, ili kuweka mfano wa reli ya China barani Afrika, reli hiyo imepangwa kwa vigezo vya matumizi ya miaka 100, na muda wa matumizi na sifa zake ni sawa na reli ya mwendo kasi nchini China. Wanataka kugombea tuzo ya Luban kwa mradi wa reli hiyo ambayo ni tuzo la kiwango cha juu zaidi kwenye sifa za miradi ya ujenzi nchini China. Anasema,

    "Reli hii ina maana muhimu sana. Hivi sasa China na nchi nyingi zinafanya ushirikiano kwenye reli. Reli hii inajengwa kikamilifu kwa vigezo vya China, kama tukifanya vizuri, reli hii itahimiza ushirikiano kati ya China na nchi nyingine kwenye ujenzi wa reli, pia itahimiza uwekaji wa vigezo vya reli. Tulipoanza utekelezaji wa mradi huu, tuliweka lengo moja, yaani kushiriki kwenye kugombea tuzo ya Luban, hivyo tumefanya kazi kwa mujibu wa matakwa ya tuzo hiyo, ili kuhakikisha mradi wetu unaweza kuwekwa kwa mtihani wa kihistoria. Vilevile tuna matumaini kuwa tutapata tuzo ya Luban kupitia jitihada zetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako