• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umuhimu wa familia kwa wachina

    (GMT+08:00) 2015-05-14 14:20:27

    Wachina kwa kawaida ni watu wa familia. Na umuhimu wa familia kwa wachina una historia ndefu, kwa tunaoishi hapa Beijing na tukitembelea sehemu za katikati ya Beijing ambazo zilikuwa na nyumba za zamani, tunaweza kuona nyumba ambazo ndani yake kulikuwa na familia hata za vizazi vitatu, yaani babu na bibi, baba na mama, na watoto wanaishi katika nyumba moja, na wengine tunasikia hata kama hawaishi kwenye nyuma moja basi, wanaishi karibu na wazazi wao au ndugu wa karibu. Kwa hiyo kwa ujumla familia ni kitu chenye umuhimu wa kipekee kwa wachina.

    Leo kwenye kipindi hiki tunaangalia familia na umuhimu wake kwa wachina, hasa katika mazingira mapya yenye changamoto zinazotokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha katika jamii ya China.

     


    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako