• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Daktari wa manowari ya hospitali "Peace Ark"

    (GMT+08:00) 2015-05-18 16:20:30

    Manowari iitwayo "Peace Ark" ni meli ya hospitali ya China inayotoa msaada wa matibabu katika nchi mbalimbali. Bw. Wang Zhihui ni daktari wa jeshi la majini la China, amefanya safari nne za meli hiyo ambayo ni hospitali inayohamahama na kutoa msaada wa matibabu katika nchi mbalimbali.


    Daktari Wang alisema katika safari hizo za kuwatibu wagonjwa wa nchi za nje, kilichompa kumbukumbu nzito ni watoto wanne waliozaliwa kwenye manowari hiyo na wazazi wao kuwapa majina ya "Peace Ark" na "China Rose".

    Kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2014, Daktari Wang Zhihui alisafiri mara nne kwa meli hiyo ya hospitali kwenda nchi 18 za Afrika, Asia ya Kusini Mashariki na Pasifiki ya Kusini kutoa huduma za matibabu. Katika safari hizo nne, daktari Wang na wenzake walisafiri kwa siku 352 na kilomita elfu 110, ambapo waliwatibu watu 72,812 na kufanya upasuaji kwa watu 647. Daktari Wang Zhihui manowari hiyo ya hospitali Peace Ark imejulikana sana duniani.

    "Hospitali ya Peace Ark iko kwenye manoari, lakini tofauti na manoari nyingine, ina rangi ya nyeupe. Vilevile imepakwa alama kubwa ya msalaba mwekundu kwenye manowari hii yenye urefu wa mita 178, upana wa mita 24 na urefu wa kwenda juu mita 35.5. Manowari hii ni kubwa, na ina uwezo wa kubeba tani 14,300. Wakati ikitia nanga bandarini, inaonekana kama msichana mtuliuvu, na wakati ikiwa baharini, inaonekana kama mpiganaji. Kwa sasa manowari hiyo inajulikana sana kama nyota maarufu. "

    Dkt. Wang Zhihui amesema, hospitali ya Peace Ark imepongezwa na kusifiwa na watu wa sehemu ilipokwenda. Mwaka 2010, Dkt. Wang Zhihui kwa mara ya kwanza aenda na meli hiyo kutekeleza jukumu la kutoa msaada wa matibabu katika nchi za nje. Katika kituo cha kwanza walitua nchini Bangladesh, ambapo madaktari watekeleza kazi za uokoaji wa dharura mara nyingi, ila ni moja tu ambayo bado anaikumbuka mpaka leo.

    "Mpaka sasa tunamkumbuka msichana mmoja aitwaye 'mchina mdogo'. Hii ilikuwa nchini Bangladesh mwaka 2010 wakati manowari yetu ilipofanya safari ya kwanza nchi za nje. Siku moja tulipokea simu ya kuomba msaada kutoka hospitali moja ya jeshi la majini la Bangladesh. Mfanyakzi mmoja wa hospitali hiyo alikuwa na matatizo ya moyo, lakini pia alikuwa mjamzito. Katika kipindi cha wiki ya 36 ya ujauzito wake alipata uchungu wa kujifungua. Mgonjwa wa moyo haruhusiwi kubeba mimba, kwani ujauzito unasababisha hatari kubwa kwa maisha yake. Baada ya kupokea simu hiyo, tuliamua mara moja kupeleka wataalamu kufanya upasuaji. Mjamzito kama yeye hawezi kujifungua mwenyewe kwa sababu ana ugonjwa wa moyo, pia presha yake ilikuwa juu. Kama atajifungua kwa njia ya kawaida, ni lazima atafariki dunia. Wataalamu wa moyo na watalamu wa uzazi na magonjwa ya wanawake walifanya upasuaji huo, na watalamu wa moyo walitoa msaada mkubwa baada ya presha ya mgonjwa huyu kupanda wakati wa upasuaji. Vilevile wataalamu walikuwa wana maoni ya tofauti, kama wanaweza kutoa dawa ya usingizi ya nusu kaputi au kwenye sehemu ndogo watakayopasua, mwishowe walichagua njia ya pili. Ingawa njia hiyo ina hatari kubwa, lakini ni nzuri zaidi kwa mjamzito huyu. Baada ya upasuaji uliochukua zaidi ya nusu saa, mtoto mmoja wa kike alizaliwa salama na mama pia alikuwa salama. "

    Dkt. Wang Zhihui hakuwaza kuwa wazazi wa mtoto huyo watampa jina la "China", kutokana na upasuaji huo ambao pia ulisifiwa sana na kutangazwa katika vyombo vya habari vya Bangladesh.

    "Baba wa mtoto huyu alitushukuru sana, na kumpa mara moja mtoto huyo jina la "Qing" kwa lugha yake, likiwa na maana ya "China". Baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyu, tuliangalia afya ya mtoto huyu kwa saa 48 na kuhakikisha hana matatizo yoyote. Mwaka 2013, manowari yetu ilienda Bangladesh kwa mara ya pili, famila ya mtoto huyu ilikuja kututembelea. Madaktari tuliofanya upasuaji mwaka 2010 tulionana nao. Tulimpima mtoto afya yake, na wazazi wake pia walipata matibabu. Vyombo vya habari vya Bangladesh vinasema mtoto huyo ni ushuhuda wa urafiki kati ya nchi yake na China."

    Dkt. Wang Zhihui anasema miaka minne iliyopita, watoto wanne walizaliwa katika hospitali ya Peace Ark. Watoto hao walipewa majina kama Peace Ark au China Rose, na wazazi wao wanatumai majina kama hayo yatawakumbusha msaada wa madaktari hao, pia wanatumai urafiki kati ya nchi yao na China utadumu daima. Hilo ndio jambo linalomfurahisha Dkt. Wang Zhihui na wenzake wote wanaotoa huduma nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako