• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Daktari Zhang Yueming na kumbukumbu yake kuhusu Guyana

    (GMT+08:00) 2015-05-18 16:25:22

    Mwezi Machi mwaka huu, naibu mkurugenzi wa idara ya jinakolojia na uzazi wa hospitali ya chuo kikuu cha Suzhou China doktari Zhang Yueming alipokea barua pepe ya salamu kutoka Guyana kwa mgonjwa wake. Ingawa Bw Zhang alirudi China zaidi ya miezi sita iliyopita, bado barua pepe kama hii inamfanya akumbuke siku ambazo alitoa msaada wa matibabu nchini Guyana.


    Kwenda Guyana ni safari ya mbali zaidi aliyowahi kuifanya Bw. Zhang Yueming. Mwezi Juni mwaka 2012, Bw. Zhang alikuwa mmoja wa madaktari 15 kutoka hospitali za miji ya Suzhou na Changshu, mkoani Jiangsu waliounda kikundi cha 10 cha madaktari cha China kuisaida Guyana,.

    "Tulipewa kazi ya kuunda kikundi cha madaktari mwanzoni mwa mwaka 2011, madaktari waliofaulu mitihani ya ngazi kadhaa na ukaguzi wa mahojiano iliyoandaliwa na idara ya afya ya mkoa, ndio waliopewa kazi hiyo. Miongoni mwa madaktari wa kikundi hicho, wanane wamepata au wanasomea shahada ya udaktari, mwalimu wangu Profesa Yang Weiwen aliwahi kwenda Zanzibar mara mbili kutoa msaada wa matibabu, alinishauri nishiriki kwenye kazi hiyo. Nilifuata ushauri wake."

    Guyana iliyoko kwenye kaskazini mashariki mwa Bara la America Kusini ni moja ya nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zaidi duniani. Kutokana na sababu za kiuchumi, wafanyakazi wengi wa matibabu wa Guyana waliacha kazi hiyo, kuna hospitali 27 na madaktari zaidi 750 nchini kote. Hospitali ya Georgetown iliyoko kwenye mji mkuu wa Guyana ni hospitali ya kiserikali ya kiwango cha juu kabisa, lakini pia inakabiliwa na hali duni ya vifaa vya matibabu na ukosefu wa wafanyakazi, na inategemea misaada ya kimataifa. Toka mwaka 1993 China ilianza kutuma kikundi cha madaktari nchini Guyana, madaktari wa China walikuwa wanafanya kazi muhimu kwenye hospitali ya Georgetown, na kusaidia idara nyingi za hospitali hiyo kuendelea vizuri. Daktari Zhang Yueming alikumbuka kuwa, mwaka 2012 yeye na wenzake walipofika hospitali ya Georgetown, hawakupata muda wa kupumzika na walianza kufanya kazi haraka.

    "Maofisa wa hospitali ya Georgetown na wizara ya afya walitaka tuanze kazi haraka iwezekanavyo. Hii ilikuwa ni changamoto kubwa kwetu, kwani bado tulisumbuliwa na tofauti ya muda na nyumbani, tulichoka sana baada ya safari ndefu na tulikuwa hatujazoea hali ya huko, lakini tulianza kazi mara moja."

    Baada ya kupita kipindi cha kuzoea maisha katika nchi hiyo geni, kazi kubwa zaidi zilikuja. Guyana inatekeleza mfumo wa matibabu ya ngazi kwa ngazi, wagonjwa waliokuja kutibiwa kwenye hospitali ya Georgetown walielekezwa na kuchaguliwa na hospitali za ngazi ya chini, na baadhi ya wagonjwa walikuwa wamesubiri kwa zaidi ya nusu ya mwaka. Kwa hivyo hospitali hiyo inawapokea wagonjwa wengi waliougua sana, na katika idara ya jinakolojia na uzazi aliyofanya kazi daktari Zhang kazi zilikuwa nyingi zaidi. Bw. Zhang Yueming ni daktari mwandamizi, mbali na kuwafanyia upimaji na kuwatibu wagonjwa waliokwenda kwake, pia alitoa ushauri kwa madaktari wengine. Katika siku mbili za kufanya upasuaji kila wiki, ili kuwatibu wagonjwa wengi zaidi, daktari Zhang alifanya kazi kutoka asubuhi hadi jioni, wakati mwingine hakuwa na muda wa kula chakula cha mchana. Hivyo wenzake wenyeji walimpa jina la mtaalamu anayekula mlo mbili tu.

    "Wagonjwa wengi walikuja hospitali kwa ndege au walipanda meli saa 10 asubuhi, kama ukichelewa kuwatibu, hawawezi kurudi nyumbani au wanapaswa kusubiri baada ya miezi mitatu. Nilipojua hali hii, nilisema inaweza nisile chakula, lakini ni lazima nimalize kazi ya kuwatibu wagonjwa. Awali idara yetu ilifanya upasuaji mara mbili tu, niliongeza hadi mara tano sita, nilifanya upasuaji kwa muda wa ziada. Wakati huo huo nilikula chakula kingi asubuhi na kula mkate na vyakula vidogo wakati niliposikia njaa."

    Guyana iko kwenye sehemu yenye joto, hali ambayo ni tofauti na China. Hivyo madaktari wa China walijikuta kukabiliwa na baadhi ya magonjwa ambayo hawajakutana nayo nchini China. Daktari Zhang Yueming akishirikiana na wenzake walifanikiwa kufanya upasuaji mgumu ambao ulikuwa wa mara ya kwanza katika historia ya matibabu ya Guyana. Bw. Zhang Yueming aligundua kuwa ingawa hospitali ya Georgetown inakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa raslimali na vifaa vya kisasa, lakini ina kiwango cha juu cha ushirikiano wa kimataifa, idara ya jinakolojia na uzazi ni kama umoja wa mataifa mdogo, ambapo wataalamu na wasomi kutoka nchi za Asia, Afrika na America Kaskazini wanakusanyika wakibadilishana maoni ya matibabu. Lakini kutokana na mawazo ya jadi na tatizo la kiuchumi, watu wa Guyana hawafuatilii sana afya ya wanawake waliojifungua na kiwango cha vifo vya watoto wachanga, ndiyo maana madaktari na wauguzi hawatilii maanani maendeleo ya afya ya wanawake baada ya kujifungua na huduma za afya kwa watoto wachanga. Kutokana na hali hii, kila siku daktari Zhang aliwatembelea hali ya wanawake waliojifungua, hatua kwa hatua mawazo ya madaktari wa China ya kulinda afya ya kina mama na watoto wanaozaliwa yalipokelewa na watu wengi wa Guyana.

    "Baada ya mtoto kuzaliwa, kazi yetu inakuwa haijamalizika. Tunapaswa kufuatilia kama hali yake ni nzuri, kama mama alitokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua. Kila siku nilitembelea wodi za uzazi na kuangalia rekodi, baada ya kugundua jambo, niliwauliza wagonjwa mara kwa mara na kutafuta tatizo liko wapi."

    Baada ya kufanya kazi nchini Guyana kwa miezi minne, Bw. Zhang Yueming alikuwa amekubaliwa kabisa na watu wa huko, hospitali aliyofanya kazi na serikali ya Guyana kutokana na uhodari wake wa kitaaluma na uchapaji kazi. Mwezi Oktoba mwaka 2012, wizara ya afya ya Guyana na hospitali ya Georgetown zilikubaliana kumteua daktari Zhang awe mkurugenzi wa idara ya jinakolojia na uzazi ya hospitali ya Georgetown, mjumbe wa tume ya ushauri ya matibabu ya hospitari hiyo na mjumbe wa kamati ya wizara ya afya ya Guyana inayoshughulikia vifo vya wajawazito na wanawake wa uzazi. Daktari Zhang alipewa kazi ya kusimamia idara ya jinakolojia na uzazi ya hospitali ya Georgetown, na kushiriki kwenye utungaji wa sera za afya za Guyana. Katika kutekeleza majukumu hayo, daktari Zhang aliongeza mafunzo kwa madaktari na wauguzi, kuimarisha ujenzi wa utaratibu wa idara hiyo, kurekebisha mchakato wa matibabu, kuboresha upangaji wa wodi za idara hiyao, kuandaa mwongozo wa ufundi wa matibabu, na kukamilisha mfumo wa usiammizi wa idara hiyo.

    "Awali nilipofanya upasuaji, msaidizi wangu hakujua namna ya kunisaidia, hivyo niliwafundisha kwa zamu, sasa nimewafundisha madaktari 18 ambao kila mmoja anaweza kutoa matibabu peke yake. Niliwafundisha madaktari wenyeji kwani hawataondoka."

    Wakati daktari Zhang alipokuwa mkurugenzi wa idara ya jinakolojia na uzazi, idadi ya wanawake wanaokufa wakati wa kujifungua kwenye hospitali ya Geogretown ilipungua sana, na mwaka 2013 kwa mara ya kwanza ilitimiza malengo ya milenia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako