• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Zhenchang na madaktari wenzake wa China walioko mstari wa mbele kukabiliana na Ebola nchini Guinea

    (GMT+08:00) 2015-05-18 16:27:15

    Naibu mkuu wa Hospitali ya Urafiki hapa Beijing daktari Wang Zhenchang ni kiongozi wa kikundi cha 24 cha China kinachotoa msaada wa matibabu nchini Guinea. Daktari Wang aliongozana na wenzake wa kikundi hicho walikwenda Guinea wakati ugonjwa wa Ebola ulipoanza kuenea katika Afrika Magharibi. Mbali na kutibu wagonjwa, alitoa mafunzo kwa madaktari wa Guinea.


    Mwishoni mwa mwaka 2013 Wang Zhenchang aliteuliwa kuwa kiongozi wa kikundi hicho.

    "Kikundi cha 24 kiliundwa na watu 19, wote walitoka hospitali ya urafiki. Hii ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kuteua naibu mkuu wa hospitali aliye kazini kuwa kiongozi wa kikundi cha kutoa msaada wa matibabu nje, naona fahari kwa kuwa mtu wa kwanza."

    Hata hivyo, wakati kazi ya kuunda kikundi ilipokamilika na walipokuwa tayari kufunga safari kwenda Guinea kubadilishana zamu na kikundi cha 23, homa ya Ebola ililipuka katika Afrika Magharibi, na Guinea ilikuwa nchi iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa huo. Katika hali hiyo, watu walianza kujiuliza kama kikundi hicho kitakwenda Guinea kama ulivyopangwa, kiongozi wa kikundi hicho daktari Wang Zhenchang alitoa jibu bila kuchelewa.

    "Nchi nyingi zilianza kurudisha uwekezaji na wananchi wao wanaoishi katika nchi tatu zilizoathiriwa vibaya na ugonjwa wa Ebola, pia tulipaswa kutoa uamuzi. Lakini kama tusingeenda, kikundi chla 23 kisingeweza kurudi nyumbani, kwani ni lazima kikundi cha madaktari wa China kipo nchini Guniea, huu ni mkakati wa taifa letu."

    Agosti 16 mwaka jana, daktari Wang Zhenchang na wenzake 10 walitangulia kufika Guinea, na kuanza kazi katika siku iliyofuata. Si kama tu walileta huduma na vifaa vya matibabu, bali pia matarajio na imani ya kushinda ugonjwa kwa watu wa Guinea waliokabiliwa na hali mbaya ya maambukizi ya Ebola.

    "Cha muhimu zaidi ni kwamba tulifika wakati wa hali mbaya ya maambukizi ya Ebola, hiki ni kitu kukubwa kwa sekta mbalimbali nchini Guinea, kuanzia hospitali hata rais."

    Mlipuko wa homa ya Ebola pia uliathiri vibaya wachina na wafanyakazi wa makampuni ya China waliopo nchini Guinea, lakini ujio wa kikundi cha matibabu kilichoongozwa na Wang Zhenpia uliwatuliza sana.

    "Ujio wetu pia uliwapa moyo wachina waliopo nchini Guinea. Waliona wanaweza kututegemea, na afya zao kulindwa na madaktari waliotoka hospitali nzuri mjini Beijing haswa wakati wa mlipuko wa Ebola. Na pia tulifungua hospitali ndogo katika eneo tuliloishi na kuwapatia bure wachina huduma za matibabu kwa saa 24."

    Daktari Wang pia alikuwa na jukumu la kuwa naibu mkuu wa Hospitali ya Urafiki ya China na Guinea. Mbali na kufanya kazi katika hospital hiyo, yeye na wenzake pia walitoa mafunzo ya afya ya umma kwa vyombo vya kiserikali vya nchi hiyo. Mafunzo kama hayo sio tu yanawawezesha watu wa Afrika kupata uzoefu wa China katika afya za umma na kuzuia na kutibu magonjwa ya kuambukizwa, bali pia yanazidisha urafiki wa jadi kati ya China na Guinea.

    "Tumetoa mafunzo kwa watu 1600 waliotoka ikulu, wizara za usalama na mambo ya nje n.k. Mafunzo hayo ni muhimu zaidi kuliko yanayotolewa kwa wahudumu wa afya. Kwani baada ya kupewa mafunzo, vyombo hivyo vya kiserikali viliweza kubadili mitazamo yao, na kuwa na mitazamo mipya juu ya ujenzi wa mfumo wa afya ya umma, na kufuata mkakati mwafaka, hii ina maana kubwa kwa udhibiti wa Ebola na magonjwa mengine ya kuambukizwa nchini humo."

    Kutokana na juhudi za Wang na mkuu wa Hospitali ya Urafiki ya China na Guinea Fode Ibrahima Camara, mafunzo hayo yalikamilishwa vizuri, na Bw Camara alikishukuru kikundi cha 24 cha matibabu kilichoongozwa na Wang Zhenchang.

    "Tumeridhika sana na msaada uliotolewa na serikali ya China na kikundi cha matibabu. Katika mchakato wa kupambana na ugonjwa wa Ebola, serikali ya China na wananchi wake siku zote wamekuwa pamoja na watu wa Guinea. Sijui ni kiasi gani cha msaada iliotoa China kwa Guinea, lakini najua walituma fedha, vitu na watu. Ujio wa madaktari wa kikundi cha matibabu cha China umesaidia sana afya zetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako