• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tabasamu la muuguzi kutoka China lachangia mapambano dhidi ya  Ebola

    (GMT+08:00) 2015-05-18 16:29:58

    Bibi Wang Jing ni muuguzi wa China ambaye yupo nchini Guinea akishirikiana na madaktari na wauguzi wenzake katika mstari wa kwanza wa kupambana na maambukizi ya ugonjwa Ebola. Mwezi wa Agosti, mwaka jana, Bi Wang alijitolea kujiunga na kikosi cha 24 kilichopelekwa na China kutoa msaada wa matibabu nchini Guinea kwa miaka miwili.


    Guinea iliyopo Afrika Magharibi ni nchi inayokumbwa mara kwa mara na magonjwa mengi ya kitropiki, kama vile malaria na homa kali. Tokea mwanzoni mwa mwaka 2014, kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa Ebola katika Afrika Magharibi, Guinea ni moja ya nchi zilizoathiriwa vibaya na ugonjwa huo. Alipofika nchini humo, Bibi Wang na wenzake walianza kazi mara moja hata walikuwa hawajazoea tofauti ya muda.

    "Tulifika Guinea wakati wa msimu wa mvua. Hali ya hewa ni joto na unyevu. Tulipofika tulianza kunyunyiza dawa za kuua virusi katika makazi yetu na hospitali tunayofanya kazi. Tukivaa mavazi mazito ya kujikinga na vifaa vya kunyunyizia dawa vyenye kilo zaidi ya 10, tulisafisha kila chumba baada ya kingine. Jasho likatoka baada ya dakika chache tu, na ilichukua saa 2 hadi 3 kumaliza kazi hiyo. Ingawa tulichoka sana baada ya safari ndefu kutoka China, tulipaswa kumaliza kazi hiyo usiku huo. Nafikiri, ilikuwa ni mazoezi mazuri kwa tabia yetu."

    Licha ya kazi hiyo, muuguzi Wang na wenzake walianza mara moja kazi ya kuwatibu wagonjwa katika hospitali ya urafiki wa China na Guinea mjini Conakry iliyojengwa kwa msaada wa China. Kutokana na hali mbaya ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola, kila mgonjwa aliyekwenda hospitali hiyo alipimwa virusi vya Ebola. Madaktari na wauguzi waliofanya kazi hapa pia walikabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo.

    "Dalili ya Ebola si homa tu, na asilimia 10 ya wagonjwa wa Ebola wanaweza kuonekana dadili zinazofanana na magonjwa mengine ambayo ni ya kawaida katika Afrika Magharibi. Katika hali hii, tunakabiliwa na hatari kubwa. Kazi ya muuguzi inahusika moja kwa moja na damu, ambayo ni njia muhimu ya kuenea kwa virusi vya Ebola, hivyo tulikuwa na uwezekano mkubwa wa kuambukizwa. Hata hivyo, nafikiria kwanza wagonjwa, na kutoa kipaumbele usalama wa wagonjwa."

    Bibi Wang alipangiwa kufanya kazi kwenye chumba cha upasuaji kwenye hospitali ya urafiki wa China na Guinea. Aliwafundisha wauguzi wengine wa hospitali hiyo ujuzi wake wa uuguzi, hasa kwa mshirika wake Bibi Mariama ambaye ni muuguzi anayefanya kazi katika hospitali hiyo kwa miaka takriban mitatu. Bibi Mariama anasema, ni imekuwa bahati kwake kukutana na Bibi Wang, na anamshukuru sana.

    "Bibi Wang ni mshirika wangu katika hospitali pia ni muuguzi mzuri sana. Yeye ni mchangamfu na hutabasamu wakati wote. Ingawa tunazungumza kwa lugha tofauti, anawasiliana nasi kwa upole na kutufundisha mbinu na ujuzi wa uuguzi. Tunajifunza mengi na kupata faraja hususan wakati huu mgumu wa maambukizi ya Ebola. Tangu afike hospitali yetu, tumeshirikiana vizuri. Nina imani kuwa, tutaendelea kushirikiana kama hivyo."

    Licha ya kazi ya uuguzi, Bibi Wang pia ni katibu katika kikosi chake. Kila siku, anaandika kumbukumbu za mikutano na ripoti za matibabu. Mara kwa mara, anafanya kazi zaidi ya muda wa kawaida.

    "Naweza kufanya kazi za ukatibu wakati wa usiku tu. Kutokana na hali duni ya mtandao wa internet nchini Guinea, ninachukua muda mrefu zaidi kuwasilisha ripoti za kazi nyumbani China. Inaweza nafanya kazi mpaka usiku sana. Baadhi ya wakati inabidi kuamka usiku wa manane kuendelea na mawasiliano ya kikazi na China."

    Kutokana na kazi nzito na uhaba wa vifaa, muuguzi Wang alishindwa kulala na kula kwa wakati, na alikuwa anajisikia shinikizo la kisaikolojia na afya yake kuathiriwa. Hata hivyo alikuwa anafanha kazi akiwa na tabasamu. Mkuu wa hospitali ya urafiki wa China na Guinea, Bw. Fode Ibrahima Camara alisema

    "Hata wakati hali ya maambukizi ya Ebola ilipokuwa mbaya sana, muuguzi Wang alikuwa anajitahidi kutoa mafunzo kwa wauguzi wa hospitali yetu, hususan namna ya kuwatunza wagonjwa mahututi. Ametusaidia sana. Wakati ule ilitubidi tusimamishe kazi hiyo ya kuwatunza wagonjwa mahututi kutokana na kukosa wauguzi. Muuguzi Wang alipofika na kujionea hali ya wodi ya wagonjwa mahututi, aliamua kuanza mara moja kutoa mafunzo hayo. Nafahamu ana kazi nyingi, kutoa mafunzo ni kazi nzito ya ziada, hata hivyo anafanya kazi kwa tabasamu. Tuna imani na uwezo wake wa kitaaluma."

    Tabasamu ndiyo ni nembo ya muuguzi huyo Wang Jing. Toka aanze kufanya kazi huko Guinea, alikuwa anawapa moyo wengine kwa tabasamu na kuwasaidia kwa vitendo vyake.

    Mwezi Februari, mwaka huu, ni majira ya joto pale Guinea, pia ni mwaka mpya wa kijadi wa China, Bibi Wang aliweka matarajio yake ya mwaka.

    "Napenda kutumia muda huu wa miaka miwili kubadilishana uzoefu na madaktari na wauguzi wenzangu wa chumba cha upasuaji, kutoa mafunzo zaidi kwa wauguzi wa Guinea, na kuwasaidia kukamlisha utaratibu wa kitaaluma. Natarajia matunda ya kazi yangu ya miaka miwili yatabaki hapa Guinea. Nikiwa na fursa, napenda kuja tena hapa. Wakati nitakapokuja tena, natarajia kiwango cha matibabu nchini Guinea kitakuwa kimepata maendeleo makubwa na watu wake kuwa na huduma nzuri ya matibabu. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako