• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dunia kunufaika na Ukanda mmoja na Njia moja

    (GMT+08:00) 2015-05-20 16:33:38

     

    Kutokana na takwimu zilizotolewa karibuni na wizara ya biashara ya China, thamani ya biashara kati ya China na nchi zilizoko kwenye ukanda wa kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri ya baharini ya karne ya 21, imefikia dola za kimarekani bilioni 236 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ambapo imechukua asilmia 26 ya thamani ya biashara kati ya China na nje. Wakati huo huo, wizara ya biashara ya China pia imesema, hivi sasa kuna zaidi ya 70 ya maeneo ya ushirikiano yanayojengwa kwenye nchi zilizoko kwenye Ukanda mmoja na Njia moja chini ya ushirikiano kati yao na China, na uwekezaji kwa miundo mbinu ya maeneo hayo utazidi dola za kimarekani bilioni 8, na kampuni zitakazoingia kwenye maeneo hayo zitawekeza dola za kimarekani bilioni 10 hivi. Na inakadiriwa kuwa thamani ya uzalishaji ya maeneo hayo itazidi dola za kimarekani bilioni 20, na maeneo hayo yatatoa nafasi za ajira laki 2.

    Takwimu za utangulizi pia zimethibitisha maoni ya pamoja ya wasomi na wataalamu waliohudhuria mkutano wa kimataifa wa maofisa waandalizi wa mashirika ya fedha uliofanyika hivi karibuni huko Shenyang, China. Kwenye mkutano huo washiriki wamejadili pendekezo la China kuhusu Ukanda mmoja na Njia moja, pia wamefikia maoni ya pamoja kuwa dunia itanufaika na maendeleo ya China.

    Naibu mwenyekiti wa benki ya kimataifa ya Raiffeisen ya Austria amesema, pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja ni muhimu sana kwa nchi zilizo kwenye ukanda huo na kando ya njia hiyo, na China na nchi hizo zinaweza kusaidiana kiuchumi. Baadhi ya wataalamu wamesema pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja ni hatua muhimu ya kuwasliana na dunia, ambalo litahimiza utulivu na usalama wa kikanda.

    Mkurugenzi wa kundi la uwekezaji wa Euro Sino amesema, Ukanda mmoja na Njia moja ni mazungumzo ya usawa, watu wote wanakabliana na fursa na changamoto za pamoja, na nchi magharibi zinapaswa kuangalia pendekezo hilo kwa msimamo wa kufungua zaidi.

    Aliyekuwa waziri mkuu wa Australia ambaye pia ni mkuu wa taasisi ya utafiti wa sera katika shirikisho la Asia la Marekani Bw. Kevin Rudd hivi karibuni huko New York amekanusha kauli kuwa uchumi wa China utadidimia, na kusema pendekezo la China la "Ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri na njia ya hariri ya baharini ya karne 21" litasaidia maendeleo tulivu ya China kwa muda mrefu. Bw. Kevin Rudd alisema,

    "Pendekezo la "Ukanda Mmoja Njia Moja" halitegemei tu sehemu za pwani za China peke yake zenye mawasiliano zaidi na nchi za nje. China inafungua sehemu nyingine zitakazofunguliwa kwa bara la Ulaya na Asia. Na sehemu za magharibi na sehemu za kusini magharibi mwa China zilizoko mbele ya kufungua mlango kwa sehemu hizo mpya, ambazo ziko nyuma kimaendeleo kuliko sehemu ya mashariki na katikati. "

    Bw. Rudd pia alikanusha kauli kuhusu mustakbali wa China utakuwa mbaya kutokana na kupungua kwa kasi ya ongezeko la uchumi wa China. Alisema kauli hiyo haina msingi wa uchunguzi na haiaminiki.

    Maofisa kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa mwaka 2015 wa safari za Anga wa Afrika unaofanyika hivi karibuni huko Dubai, wamesema pendekezo la China kuhusu Ukanda Mmoja na Njia Moja litaongeza uwekezaji wa China barani Afrika na kuiletea Afrika wasafiri wengi zaidi kutoka Asia.

    Waziri wa uchukuzi wa Ghana Bi. Dzifa Aku Attivor amesema, nchi yake inakaribisha China kujiingiza zaidi kwenye soko la safari za anga barani Afrika ambalo bado halijaendelezwa. Amesema Afrika ina asilimia 12 ya idadi ya jumla ya watu duniani, lakini soko la safari za anga barani humo linachukua asilimia 1 tu. Ameongeza kuwa, Ghana iko wazi kwa biashara, na inakaribisha mapendekezo yoyote yanayoweza kuiunganisha Asia na nchi nyingine duniani, ikiwemo pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, ambalo lilitolewa na rais Xi Jinping wa China mwaka 2013.

    Mwenyekiti wa Shirika la Ndege la Rwandair, ambaye pia ni mkurugenzui mtendaji wa zamani wa Shirika la Ndege la Ethiopia Girma Wake amesema, China imesaidia kudhibiti gharama za ndege na viwanja vya ndege barani Afrika. Amesema kwa viwanda vya Ethiopian, China ni chanzo muhimu cha soko la vipuri na bei za bidhaa muhimu zinazotengenezwa nchini China ni chini kwa asilimia 30 ikilinganishwa na sehemu nyingine duniani. Akizungumzia Ukanda Mmoja na Njia Moja, Wake amesema pendekezo hilo litainufaisha China na kuinua tabaka la kati, hali ambayo itailetea Rwanda watalii na wafanyabiashara wengi zaidi wa China .

    Naye mkuu wa Viwanja vya Ndege vya Dubai ambavyo vinamilikiwa na serikali Paul Griffiths amesema, Dubai itafanya kazi muhimu ya kuiunganisha Afrika na dunia katika ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri, na kutolea mfano wa mashirika 13 ya ndege barani Afrika yanayofanya safari zake kupitia Dubai, ambazo zinakwenda viwanja 29 katika nchi 20. Amesema Dubai iko kwenye eneo muhimu kati ya Afrika na Asia, na idadi ya abiria kutoka na kwenda Afrika kutokea Dubai imeongezeka na kufikia milioni 6.5 kwa mwaka.

    Naye Xu Bo, ofisa wa ngazi ya juu katika kampuni ya safari za anga na ulinzi inayomilikiwa na serikali ya China, AVIC amesema siku zote China imejaribu kushirikiana na nchi za Afrika chini ya msingi wa kunufaishana. Ameongeza kuwa, mahitaji ya ndege ndogo za abiria zinazotengenezwa na China kama vile Xian MA-60 yenye viti 56 na Harbin Y-12 yenye viti 19 yanaongezeka kwa kasi kwenye safari za ndani ya nchi za Afrika.

    Tawanda Gusha, mkurugenzi wa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Zimbabwe amesema, nchi yake inakaribisha wawekezaji kutoka China, na anatumai kuwa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja litaongeza nguvu ya sekta ya usafiri wa anga barani Afrika.

    Griffiths amesema, anapenda kutoa ushauri kwa nchi zilizo kwenye eneo la ukanda wa kiuchumi wa njia hariri ni kuendelea kuwekeza kwenye viwanja vya ndege na uwezo wa ndege zao, kwa kuwa pendekezo la China litachochea ongezeko kubwa zaidi la abiria itakapofika mwaka 2030 katika eneo kati ya Afrika na Asia-Pasific.

    Mwaka jana, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai ulichukua nafasi ya uwanja wa ndege wa Heathrow, London, na kuwa uwanja unaopokea abiria wengi zaidi wa kimataifa duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako