• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juhudi za China katika kupunguza maafa

    (GMT+08:00) 2015-05-21 15:03:34

    Hivi karibuni China imefanya shughuli mbalimbali za kuadhimisha siku ya 7 ya kupambana na kupunguza maafa, na mwaka huu kauli mbiu ilikuwa "matumizi ya njia za kisayansi kupunguza maafa". China ni nchi yenye eneo kubwa sana la ardhi. Na ni nchi ambayo inakumbwa mara kwa mara na changamoto za kimazingira na hata majanga ya kimaumbile. Kwa wakati mmoja unaweza kusikia kuwa mkoa mmoja unasumbuliwa na baridi kali, mwingine unasumbuliwa na mafuriko na mwingine unasumbuliwa na ukame, na wakati mwingine kimbunga au tetemeko. Kutokana na ukubwa wa eneo kubwa ardhi iliyopo kwenye maeneo tata kimaumbile ya asili, China ni moja kati ya nchi zinazokumbwa na maafa makubwa ya asili. Mfano wa majanga makubwa yaliyotokea miaka ya karibuni ni tetemeko kubwa la ardhi la mji wa Wenchuan mwaka 2008, lililosababisha vifo vya watu karibu elfu 70. Janga hilo lilifanya wachina waanze kujadili namna na kujikinga na kupunguza maafa inapotokea janga kubwa kama hilo. Kwa undani zaidi hebu sikilize kipindi chetu.

     


    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako