• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa CICA wafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2015-05-25 17:03:21

    Mkutano wa kwanza wa mwaka wa Baraza lisilo la kiserikali la Mkutano kuhusu Maingiliano na Hatua za Kujenga Uaminifu Barani Asia CICA umeanza leo hapa Beijing.

    Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, naibu mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng amesema, huu ni mwaka wa 70 tangu ushindi wa vita dhidi ya Ufashisti duniani, na katika miaka 70 iliyopita, hali ya usalama barani Asia imekuwa tulivu, na maendeleo makubwa yamepatikana. Amesema msingi wa utulivu wa maendeleo ya Asia unatakiwa kuimarishwa zaidi, na bado kuna safari ndefu na changamoto kubwa kwa Asia kutimiza amani ya kudumu na maendeleo ya pamoja.

    Bw. Yu ameongeza kuwa katika mwaka mmoja uliopita tangu China iwe nchi mwenyekiti wa CICA kuanzia 2014 hadi 2016, imetekeleza kwa makini majukumu yake na kufanya kazi kubwa katika kuhimiza hatua za kujenga uaminifu katika maeneo mbalimbali ndani ya CICA na kupanua mawasiliano kati ya CICA na nje. Amesema China itaendelea kujadiliana na pande mbalimbali katika masuala yanayohusu usalama na maendeleo, na kuongeza uwezo wa utekelezaji wa nchi hizo katika kukabiliana kwa pamoja na matishio na changamoto za kiusalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako