• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za kutengeneza magari za China zatilia maanani uvumbuzi

    (GMT+08:00) 2015-05-27 15:19:40


    Kampuni ya kutengeneza magari ya China Chery ambayo inauza magari kwa wingi zaidi nje ya nchi itawekeza mamilioni ya dola za kimarekani kujenga kituo cha utafiti na maendeleo cha ngazi ya dunia katika miaka mitano ijayo.

    Mwaka jana, kampuni hiyo iliuza magari laki 1.1 nje ya China, idadi ambayo imeifanya ishike nafasi ya kwanza kwa mauzo ya nje kwa miaka 12 mfululizo. Kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1997 na yenye makao yake makuu mkoani Anhui, kusini mwa China, imeuza magari milioni moja duniani tangu ifanikiwe kutengeneza gari lake la kwanza mwishoni mwa mwaka 1999.

    Mwenyekiti wa Chery Yin Tongyue amesema, ili magari yaweze kuingia kwenye soko la kimataifa, chapa na ubora ni muhimu.

    Kwa muongo, kila mwaka kampuni hiyo iliwekeza asilimia saba ya mapato ya mauzo katika shughuli za utafiti na maendeleo, na katika miaka kadhaa, uwekezaji huo uliwahi kufikia asilimia 10.

    Oda ya kwanza ya magari kumi ilitengenezwa na Chery ilitoka kwa wateja nchini Syria mwaka 2001, na kampuni hiyo ilitumia fursa hiyo kuanza safari zake za "kutoka nje".

    Wakati huohuo, Chery imegundua kuwa ili chapa yake iwe ya kimataifa zaidi, ni lazima kufanya ushirikiano wa kimataifa katika mzunguko kamili wa viwanda, kutumia ipasavyo rasilimali zenye nguvu duniani, kuinua uwezo wa kuvumbua ili kuwa na soko kubwa zaidi la kimataifa.

    Yin amesema kampuni yake imeunda ushirikiano na Bosch, Bayer na kampuni nyingine kumi zenye nguvu duniani ili kuendeleza teknolojia ya injini, tekonolojia ya nyenzo mpya, mapambo ya ndani na nje na nyingine zinazohusika na sekta mbalimbali zilizopo katika mambo yote yanayohusiana na magari.

    Kadri Chery ilivyopata maendeleo na uzoefu katika uvumbuzi wa teknolojia muhimu na utengenezaji wa vipuri muhimu vya magari pamoja na mambo yote yanayohusu magari, ndivyo inavyobadilisha mkakati wake kutoka kuuza magari hadi soko la kimataifa hadi kuingia soko linalolengwa", na imeanza kujenga viwanda katika masoko muhimu duniani.

    Tukio muhimu kwa mkakati wa kimataifa wa Chery lilikuwa ni uzinduzi wa kiwanda chake kinachojiendesha nje ya China mwaka 2014, ambapo Chery ilijenga kiwanda cha kutengeneza magari na injini nchini Brazil na kuwekeza dola za kimarekani milioni 22.3 kujenga kituo cha utafiti na maendeleo katika nchi hiyo ya Amerika Kusini, hatua ambayo ilimaanisha kuwa Chery iliingia kwenye kipindi kipya cha kutengeneza magari moja kwa moja katika nchi za nje.

    Meneja mkuu wa kiwanda hicho nchini Brazil Peng Jian amesema asilimia 70 ya wafanyakazi ni wenyeji, na idadi hiyo inatarajiwa kufikia asilimia 90. Amesema kiwanda cha Chery nchini Brazil kinazingatia teknolojia isiyochafua mazingira na yenye ufanisi, maingiliano ya kitamaduni, na kutengeneza bidhaa kama wenyeji. Katika siku za baadaye, matawi ya kiwanda hicho yanatarajiwa kujengwa karibu na hapo, na kukusanya kampuni zinazouza vipuri vya magari, ili kufanikisha utengenezaji wa magari nchini Brazil kama wenyeji kwa kutimiza mzunguko kamili wa kiviwanda.

    Brazil inashika nafasi ya nne duniani kwa soko la magari, na nafasi ya sita kwa utengenezaji wa magari. Kampuni kubwa za kutengeneza magari duniani kama vile General Motors zimejenga viwanda nchini humo.

    Katika siku za baadaye Chery inapanga kufanya kiwanda chake nchini Brazil kuwa kituo muhimu cha utengenezaji katika Amerika Kusini, na kupanua soko la kanda hiyo ili kuleta nafasi nyingi za ajira na kukuza uchumi wa huko.

    Mpaka sasa, Chery imeingia katika masoko ya Asia, Ulaya, Afrika na Latin Amerka, na magari yake yanapatikana katika nchi na sehemu zaidi ya 80 duniani. Chery ina viwanda 16 vya kutengeneza magari, maduka 1,100 na vituo 900 vya huduma katika nchi za nje.

    Mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ya China kwenye ripoti yake ya kazi inayotolewa kila mwaka, imeweka bayana kwamba, inahamasisha kampuni kujiunga na kazi za ujenzi wa miundombinu nje ya nchi na kutoa uungaji mkono wa kisera na kifedha kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa katika sekta kama vile reli, nguvu ya umeme, mawasiliano ya simu, uhandisi, magari, na ndege. Kauli hizo na hatua zinazofuatwa zimezipa moyo Chery na kampuni nyingine za utengenezaji magari za China.

    Yin amesema kufanikiwa kuuza bidhaa nje ya China hakumaanishi kuwa kampuni hiyo imekuwa chapa ya kimataifa, na ni lazima kujihusisha na kuboresha mnyororo wa thamani duniani ili kuwashawishi wateja kwa ubora wa bidhaa zako.

    *****************************************

    Kwa mujibu wa makadirio yaliyotolewa na Shirikisho la Sekta ya Magari la China, mwaka huu, kasi ya ongezeko la uzalishaji na uuzaji wa magari itafikia asilimia 7, idadi ambayo itazidi milioni 25, na kuweka rekodi mpya ya kihistoria.

    Katika maonyesho ya magari ya Shanghai ya mwaka 2015 yaliyofungwa hivi karibuni, kampuni mbalimbali za kutengeneza magari za China zimeonesha aina mpya za magari, na kuongezeka kwa uvumbuzi kumefuatiliwa na wadau wa sekta ya magari.

    Kama Chery, Great Wall ni kampuni nyingine ya kutengeneza magari nchini China, na katika kibanda chake katika maonesho ya magari ya Shanghai ya mwaka 2015, magari yaliyoonyeshwa yote ni ya aina ya SUV. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Wang Fengying anasema,

    "Tumerekebisha mkakati wetu, na katika miaka miwili ijayo, kampuni yetu haitatoa magari mapya, na badala yake tutatumia nguvu zote katika magari ya aina ya SUV."

    Wang anasema kampuni hiyo itatumia nguvu zaidi katika utafiti na maendeleo ya teknolojia, na kuinua ubora wa magari yake.

    "Ubora na teknolojia vinahusiana kwa karibu. Uvumbuzi wa teknolojia unaweza kuinua uwezo na ubora wa magari. Kama ubora unainuka, inaweza kuthibitisha kuwa teknolojia iko mbele. Tunatumia nguvu zaidi katika uvumbuzi wa teknolojia kwa magari aina ya SUV, na daima ubora na teknolojia ni vitu vinavyopewa kipaumbele kwa magari hayo."

    Mwaka huu, kampuni ya magari ya Great Wall inatarajiwa kutoa aina tatu za magari ya SUV, kuboresha huduma zake baada ya mauzo, na kujenga chapa ya magari aina ya SUV ya kampuni hiyo kuwa ya kimataifa kupitia utafiti na maendeleo pamoja na huduma bora.

    Katika miaka ya karibuni, China imefanya magari yanayotumia nishati mpya, uhifadhi wa nishati, na matumizi ya nishati safi kuwa sekta mpya ya kimkakati ya taifa. Meneja wa idara ya mahusiano ya umma ya kampuni ya kutengeneza magari ya BYD ya China Du Guozhong anasema, katika maonyesho ya magari ya Shanghai ya mwaka huu kuwa, magari yao yote yaliyoonyeshwa yanatumia nishati mpya.

    "Magari yote tisa ya BYD yaliyoonyeshwa katika maonyesho ya mwaka huu ni yale yanayotumia nishati mpya. Sisi ni chapa ya kichina, hivyo magari hayo yamepewa majina ya enzi kwenye historia ya China, hii ni rahisi kwa watu kukumbuka, na pia tutakapouza magari nje ya nchi, wageni wanaweza kujua hii ni chapa ya kichina."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako