• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la 15 la sanaa la kimataifa la Meet In Beijing lamalizika

    (GMT+08:00) 2015-05-28 16:43:47

    Tamasha kubwa la sanaa la kimataifa Meet In Beijing linafanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 23 Aprili hadi tarehe 30 Mei. Katika kipindi cha leo, tutazungumzia tamasha hilo kubwa la sanaa nchini China.

    Tamasha la sanaa la kimataifa Meet in Beijing ni moja ya matamasha makubwa ya sanaa nchini China, ambalo kila mwaka wasanii kutoka nchi na sehemu mbalimbali duniani hualikwa kuonyesha utamaduni wao wa kipekee hapa Beijing katika kipindi cha mwezi mmoja hivi, na tamasha hilo litakalomalizika kesho ni la awamu ya 15. Tamasha la mwaka huu limeshuhudia makundi 42 ya wasanii na bendi 104 za muziki kutoka nchi na sehemu 25 duniani zikifanya maonesho zaidi ya 100 ndani ya kumbi mbalimbali na mengine 50 kwenye viwanja vya wazi.

    Tamasha hilo lilizinduliwa kwa maonsho ya dansi ya Ballet 'Swan Lake' iliyochezwa kwa pamoja na wachezaji mashuhuri wa Ballet wa China na Marekani.

    Kwaya ya chuo kikuu cha Brigham Young cha Marekani, ambacho ni moja ya vyuo vikuu vikubwa binafsi nchini humo, imewahi kufanya maonesho zaidi ya 30 nchini China. Kwenye tamasha la mwaka huu, kwaya hiyo imeonesha ustadi wake hodari kwa kuimba nyimbo za mitindo mbalimbali tofauti kama vile za mapokeo (Claasical), za jadi (Folk) na Broadway.

    Makundi mengine ya wasanaii kutoka Marekani ni pamoja na kwaya ya Georgia Boy, William and Mary Wind Ensemble na kundi la Ballet la Richmond.

    Bw. Isao Tomita, msanii mashuhuri wa muziki wa kielectroniki kutoka Japan, ni mmoja wa wasanii muhimu walioshiriki kwenye tamasha hilo. Mtunga muziki huyo mwenye umri wa miaka 82 ambaye alizaliwa mjini Tokyo na kuishi maisha ya utotoni nchini China akiwa na baba yake, alionesha kazi yake kubwa ya simfoni iitwayo Ihatov kwenye maskani yake ya pili nchini China.

    Mbali na wasanii hao hodari kutoka Marekani na Japan, washiriki wanaovutia zaidi kwenye tamasha hilo ni wachezaji wa dansi na wanamuziki kutoka nchi za Latin Amerika na Caribbean, ambao wameonesha utamaduni wao maalumu na uchangamfu mkubwa kwenye jukwaa.

    Maonesho ya sanaa za Latin Amerika na Carebbean yana sehemu mbili, moja ni maonesho ya dansi za aina mbalimbali zikiwemo tango, rumba, chacha na salsa, sehemu nyingine ni maonesho ya muziki yaliyoshirikisha wanamuziki kutoka Argentina, Colombia, Costa Rica, Cuba, Chile na Peru.

    Bw. Sebastian ni mchezaji mkuu wa dansi ya kampuni ya Tango Desire kutoka Argentina, anasema anatarajia kucheza tango mbele ya watazamaji wa China.

    "Dansi ya Tango ilivumbuliwa na kuendelezwa nchini Argentina. Bila shaka, mwanzoni iliathiriwa sana kutokana na uhamiaji. Sasa tunacheza tango ya aina zote, kila aina inawakilisha kipindi kimoja katika historia ya nchi yetu. Tunakuja kuonesha utamaduni na historia ya Argentina."

    Swing Latino ni kundi la dansi ya Salsa kutoka Colombia, wachezaji dansi wa kundi hilo walionesha ustadi wao mkubwa wa dansi hiyo iliyoongezewa vitendo vigumu vya mwili, ambavyo vilikuwa vikipigiwa makofi na kushangiliwa mara kwa mara.

    Bw. Luis Hernandez ni maneja wa kundi hilo, alipofahamisha dansi ya salsa anasema:

    "Salsa si dansi inayochezwa nchini Colombia pekee, lakini mji wa Cali nchini Colombia umetambuliwa kimataifa kuwa chanzo cha asili cha salsa. Dansi hiyo ni urithi wa kitaifa wa nchi yetu na inaweza kuwakilisha utamaduni wetu na maisha ya kila siku. Kwa kweli, Salsa si ngumu kama inavyofikiriwa. Wanaojifunza dansi hiyo wanaweza kufahamu umaalumu wa wenyeji wa Colombia."

    Mbali na dansi, muziki ni kivutio kingine kwenye maonesho hayo. Maonesho ya muziki wa Latin Amerika na Caribbean yaliyoanzia tarehe 1 hadi 3 Mei ni sehemu moja muhimu kwenye tamasha la Meet in Beijing la mwaka huu, na kuvutia mashabiki wengi nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako