• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kupanga vizuri maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika kipindi cha 13 cha miaka mitano

    (GMT+08:00) 2015-05-28 19:48:43

    Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na wakuu wa miji na mikoa saba ya China kwa lengo la kusikiliza maoni na mapendekezo yao kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha 13 cha mpango wa miaka mitano.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, kipindi cha mpango wa awamu ya 13 kuhusu maendeleo ya miaka mitano ni cha muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China. Serikali za ngazi mbalimbali zinapaswa kufahamu hali ya jumla na kuelewa kwa undani mwelekeo wa maendeleo ya ndani na nje ya nchi, na kuchunguza mazingira ya maendeleo ya uchumi ya ndani na nje ya nchi. Pia zinapaswa kufahamu vizuri mwelekeo na lengo la maendeleo, pamoja na fursa na changamoto zinazoikabili China, ili kutumia njia nzuri na kuepuka mbaya, na kupanga vizuri kazi za kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwenye kipindi cha 13 cha miaka mitano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako