• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Teknolojia ya hali ya juu yasaidia kampeni ya 'Fox Hunt 2015' kuwanasa raia wa China waliokimbia nchi

    (GMT+08:00) 2015-05-28 20:25:06

    Matumizi ya Big data, teknolojia ya kutambua sura, na teknolojia nyingine katika operesheni ya Fox Hunt 2015 ya China yamesaidia kuwanasa wachina waliokimbilia nchi za nje.

    Ripoti iliyochapishwa kwenye gazeti la People's Daily la China imesema, wengi wa watuhumiwa hao walikuwa wanaishi kwa kutumia majina ya bandia, hivyo kuwa vigumu kuwapata, hata hivyo, kwa kutumia teknolojia, polisi mjini Shanghai wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja.

    Mwezi Machi, mwanaume wa kichina aitwaye Zhang aliingia nchini China akiwa na hati ya kusafiria ya Australia. Kwa kutumia teknolojia ya kutambua sura na taarifa nyingine, polisi waligundua kuwa mtu huyo jina lake halisi ni Xie Renliang ambaye alikimbilia nje ya nchi mwaka 1997 alipokuwa akikabiliwa na mashtaka ya udanganifu wa kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako