• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Ban Ki-moon azitaka nchi mbalimbali ziunge mkono zaidi operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2015-05-29 16:59:22

    Leo ni "siku ya wanajeshi wa kulinda amani". Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amesifu mafanikio waliyopata walinzi wa amani, na kuzitaka nchi wanachama wa Umoja huo, hasa nchi zilizoendelea, kuunga mkono zaidi operesheni za kulinda amani za Umoja huo.

    Ban amesema, operesheni za kulinda amani zinazofanywa na Umoja wa Mataifa zimetekeleza kihalisi "katiba ya Umoja wa Mataifa". Baada ya mapambano na kujitoa mhanga kwa miongo kadhaa, helmet za bluu ambazo ni alama ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, imekuwa ishara ya matumaini kwa maelfu ya watu wanaokabiliwa na vita.

    Ban Ki-moon amesema, Umoja wa Mataifa umeanzisha vikosi 71 vya kulinda amani zilizowashirikisha askari zaidi ya milioni moja, ambao walitoa mchango mkubwa kuzisaidia nchi mbalimbali kutimiza demokrasia, kufanya uchaguzi, kulinda usalama wa raia, kuhakikisha haki za binadamu, kuhimiza utawala wa kisheria na kuwasaidia wakimbizi warudi nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako